Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
- Thread starter
- #21
🤣🤣Nahuzunuka timu ninayoishabikia (Baltimore Ravens) imetolewa. Kwa sababu tumetolewa na Kansas City Chiefs, nitakuwa naishabikia San Francisco 49ers kushinda Lombardi trophy lol.
Ninaishi Marekani toka 1996. Hata kama hushabikii American football, hii mechi haiepukiki (kuanzia wiki moja kabla ya mechi). Hata news channels zinaizungumzia. Wamarekani zaidi milioni 100 kwa wastani wanaiangalia mechi. Kwahio hata kama timu yako imetolewa, huna ujanja, lazima uiangalie. Wasio wapenzi sana wa mchezo wanafuatilia kutokana na halftime show ambayo wanamuziki mashuhuri hutumbuiza (kwa mwaka huu ni Usher).
Kiufupi, nimeipenda Ravens kwa sababu hizi. Nilikuwa siujui kabisa huu mchezo kabla sijahamia. Baada ya miaka michache, nikaanza kuufuatilia. Nikawa naangalia hususani wakati defensive players kama linebackers na centers wanapowagonga (tackle) kwa nguvu wachezaji. Wakati huo Ravens ndio wanawasajili akina Ray Lewis na Ed Reed. Hawa ni kati ya wachezaji bora wa ulinzi kuwahi kucheza. Wakati huo, hamna sheria za kumlinda mchezaji. Na akina Ray Lewis walikuwa hawana masihara na ku tackle. Ndio mapenzi yangu na Ravens yalipoanza na ni mshabiki mpaka leo. Wanajulikana sana kwa defense, ilihali miaka ya hivi karibuni offense yao imekuwa nzuri pia kutokana na Lamar Jackson. Hopefully, we shall go all the way next season.
Go Ravens!!!
Man, what happened to your Ravens?
They saw Patrick Mahomes and they froze!
And it’s not like the chiefs played super well.
They only scored 17 points. All in the first half. In the second half they didn’t score anything. And you still lost the game. What a letdown.
Lamar Jackson just ain’t that dude. The Ravens will never win the chip with him.