GE2025 Super Feo amla kichwa Dkt Mhagama Madaba Kura za Maoni

GE2025 Super Feo amla kichwa Dkt Mhagama Madaba Kura za Maoni

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Wild Flower

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2023
Posts
977
Reaction score
1,966
Madaba, Songea – Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Madaba, Mhe. Dkt. Joseph Kizito Mhagama, ameshindwa kutetea nafasi yake ya ubunge baada ya kushindwa katika mchuano wa kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Katika matokeo yaliyotangazwa na Katibu wa CCM Wilaya ya Songea Vijijini, Comrade Juma Nambaira, Dkt. Mhagama alipata kura 781, huku mpinzani wake mkuu, mfanyabiashara maarufu wa magari mkoani Ruvuma, Ndugu Omary Msigwa—anayefahamika zaidi kwa jina la Super Feo—akitwaa ushindi kwa kupata kura 1,978. Ushindi huo unamuweka Super Feo mbele kwa asilimia 68.97 ya kura zote zilizopigwa.
 
Kungekuwa na katiba nzuri inayoheshimiwa na kusimamiwa na sheria na Reforms kwenye process za uchaguzi, Wapinzani hasa Chadema wangeshiriki mwaka huu wangeshinda majimbo mengi hata urais maana samia ni mwepesi sana kwa Lissu na watanganyika Wengi hawamtaki sa100. Watu wanalazimishwa kumpenda lakini yeye hapendeki maana hajawahi kumtetea wananchi wa hali ya chini(wanyonge)
 
Gerson Msigwa yupo nyuma hili mkuu
Hata km bila Gerson, super feo alishakua na mtandao mkubwa huko chamani, unajua kua kwenye kampuni yake ya mabus wako vigogo 3 anashirikiana nao, akiwepo ke m1. Lol
 
Back
Top Bottom