Super League(AFL) imekuja kuharibu ushindani wa league za ndani.

Super League(AFL) imekuja kuharibu ushindani wa league za ndani.

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
9,189
Reaction score
16,128
Moja ya sababu kubwa inayofanya timu za ndani kung'ang'ania kushika nafasi za juu ni kucheza mashindano ya kimataifa. Sasa leo CAF wamekuja na mashindono makubwa yanayohusisha timu kutokana na points zao za CAF. Matokeo yake timu inaweza kuwa ya mwisho kwenye ligi yao lakini inaweza kushiriki AFL sabau ina points nyingi za CAF. Hii imekuja kupunguza ushindani wa ligi za ndani na kuharibu ligi zetu.
 
Eti kwa maelezo yao ni kwamba haya mashindano tana hadhi ya juu kuliko ligi ya mabingwa hapa Africa...maajabu kwa kweli.

Yaani hata enyimba, iliyotamba kwa mwaka m1 kama sio miwili miiaka kama 7 iliyopita eti nayo itashiriki...
Motsepo...Mungubanakuona.
 
Motsepe ni mpuuzi sana kapewa rushwa na infantino kafosi kuharibu soka la africa. Hayo mashindano ya super league uefa wameyakataa. Asia wameyakataa , america wameyakataa.

Yaani vyama vya soka vya mabara yote duniani wameyakataa.. yeye amefosi yawepo africa ili aibebe mamelodi yake.

Timu mpya zitakuwa hazipati nafasi hata zikitwaa ubingwa kwenye ligi za nchi zao.
 
Haijapitishwa hii, kikao hakikukaa hata nusu saa wajumbe walikataa huu ujinga, mwakani cafcl ipo na cafccl(shirikisho) ipo, hebu jitahidini mue kwanza na uhakika na habari ndo mlete huku
Na AFL ipo?
 
Back
Top Bottom