Super League kuwa na timu 24 sio timu 8

Super League kuwa na timu 24 sio timu 8

Mwanayanga hana haki ya kuanzisha mada hapa JF?

Kwani katika comment yangu imeandikwa chochote kuhusiana na haki juu ya mtu yoyote?

Au kutambulisha mtu kutokana na timu anayosupport nalo ni kosa?
 
Hilo halina ubishi na ukweli kwamba wataanza na timu nane sababu ya ratiba. Hata zitakapoanza timu 24 karia amesema wazi hajui ni vigezo vp caf itatumia kuongeza timu haina garantee tanzania itatoa timu ngapi.
zitaanza timu 24, timu 8 per region (north, central-west na southern-east)
 
Wale wanyonge 16 walioongezwa wacheze mtoano zibaki timu nane. Hizo 8 ziungane na nane kubwa za awali kutengeneza makundi 4 ya timu nne nne. Kila kundi litoe timu 2 zitakazoingia robo fainali. Kisha nusu fainali na fainali. Ila kila kundi liwe na kituo na ni mechi moja moja tu kama kwenye kombe la dunia. Hapo tutafaidi sana!!
 
Nimemsikiliza vizuri san karia leo akihojiwa efm. Yeye ameleta mrejesho wa wakati wa maamuzi waliyofanya south.
Hayo mapendekezo caf waliahidi kjyafanyia kazi lkn caf walipendekeza timu nane tuu. Hata karia leo amesema anaamini caf wataanza na 24 kwa kuwa bado wanaendelea kuwashawishi.

Caf kupitia katibu wake mkuu ambae alikuwa na kikao na naibu waziri wa michezo, mwana fa iliweka wazi kwamba wataanza na timu nane kwanza. Hii ilifiatia ombi la mwanafa kuiombea nafasi yanga hapo majuzi. Yule kigogo alimwambia wazi kwamba caf itaanza na timu nane na tayari maandalizi yamekwisha kamilika. Yanga labda watafikiriwa awamu nyingine.

Hii nguvu kubwa inayotumiwa na wachambuzi uchwara kuleta ajenda za kulazimisha ukubwa wa yanga hauna mantiki wala tija. Vilabu vingine vyote vimeheshimu maamuzi ya caf isipokuwa utopolo. Shida ni nini ukubwa haupo mitandaoni, unaonekana viwanjani.
Viongozi wetu bana yaani unapewa nafasi kukutana na mamlaka wewe unaanza kutafutia Yanga connection
 
Na hapo Kagame lazima ahakikishe ameingiza timu yake. Nguvu inayotumiwa na wanasiasa kuhakikisha Yanga anaingia ni kubwa sana utafikiri nchi haijahakikishiwa ushiriki wa timu. Yanga wanaweza kuingizwa lakini sidhani kama wame "earn" hiyo nafasi.
Apr lazima iingie ni hatari
 
Back
Top Bottom