Supercar kutoka BYD: YangWang U9 zinaanza kufanyiwa delivery hivi karibuni

Supercar kutoka BYD: YangWang U9 zinaanza kufanyiwa delivery hivi karibuni

Mad Max

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
26,961
Reaction score
77,890
Kampuni ya kutengeneza magari kutoka China Build Your Dream (BYD) wametangaza kua wale wote waliolipia (nunua) supercar yao YangWang U9, wakae mkao wa kula, sio muda zinawafikia.
2024_Yangwang_U9_side_view.png

Kama haitoshi, kila owner ataona expected delivery date aliyopangiwa katika official App ya YangWang na ikitokea tarehe aliyopangiwa kupata gari imevuka, basi BYD wata compensate kwa kumpa $28 kwa kila siku itakayozidi tokea tarehe waliyomoangia. Hizi hela hazitakuja cash, zitakuja kwa mfumo wa pints ambazo mmiliki wa gari ataweza kuzitumia katika service ya gari.
pixelcut-export-4-7.jpeg

Hii supercar inayouzwa $232,000 tu, ina acceleration kali ya sekunde 2.4 tu kutoka 0-100 km/h na top speed ya 309 km/h. Drive terrain yake ina motors nne zinazotoa horsepower 1200 na ikiwa na battery la 80 kWh litakalo kufikisha maximum range ya kilometa 450 (kama Dar to Dodoma), na ikiwa na uwezo wa kupokea fast charge (30% ya battery kwenda 80%) ndani ya dakika 10 tu, wakati slow charges (level 1 za nyumbani) itajaa kwa masaa 7 kutoka 30-80%.
pixelcut-export-5-3.jpeg

Ndani sio haba, kuielezea ni ngumu ila unaweza kujionea picha hapa chini.

pixelcut-export-18.jpeg
images (6).jpeg

Kama umependa muonekano wa iki kigari, sio kosa lako. Designer wake ni Wolfgang Egger, uyu jamaa alikuaa chief designer wa brands kubwa kama Alfa Romeo, Audi, Lamborghini.
Wolfgang_Egger_IAA_2023_1X7A0153.jpg

Ngoja tuendelee kusubiri deliveries.
 
Aiseeee!!!! Hii dunia ya magari inaenda kutekwa na wachina, nchi nyingi za ulaya walijitahidi Sana kuzuia magari ya UMEME ya kichina kama nchi ya ufaransa wao walipiga marufuku kuingiza magari Toka china lkn mwisho wa siku baadhi ya dealers walikuwa wanaingiza magari ya kichina kutoka Spain.

Hii kampuni ya BYD(build your dream) ndiyo imeaminiwa ulaya yote Kwa magari Bora, baada ya miaka 10 hawa jamaa watateka soko lote la magari duniani.
Sidhani kama kuna supercar za ulaya za EV zinaweza kupiku hiyo ndinga kuanzia bei na design
 
Back
Top Bottom