Supermarket za Shoppers kukosa chenchi

Supermarket za Shoppers kukosa chenchi

Madcheda

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2009
Posts
423
Reaction score
69
Wadau kumekuwa na nini kwenye hizi supermarket maana kila ukienda pale hawana chenchi na wanakulazimisha wabaki na hiyo chenchi. Mfano umefanya manunuzi imebaki sh 400 au 700 hawatakurudishia watasema huwana chenchi wakitegemea usamehe hiyo hela.
 
Nunua pipi pelekea watoto

Hizo tsh. 400 zikiachwa na wateja buku ni kiasi gani?

Ndio shida inaanzia hapo serikali inakosa hadi kodi
 
Sio Shoppers tu, hata Home City tawi la Mikocheni, ndani ya Jengo la Palm-village... Nafkiri kuajiri hivi vibinti vidogovidogo vyenye tamaa ya pesa za burebure vitawaharibia hawa jamaa sifa na biashara. Nafkiri wahusika waliangalie hili kwa kina na kuweka katazo.

Nitoe kisa kimoja... Siku moja, nilinunua bidhaa fulani ndani ya Shoppers Supermarket tawi la Mlimani City..., pale nilipokuwa nalipia nikakuta mabinti wawili. Namna walivyokuwa wakinisemesha na kunilegezea macho inaonesha wazi ni lugha nyingine iliyokuwa inamaanisha niwaachie ile change (kiasi kilichobaki baada ya kufanya malipo ya bidhaa niliyonunua)

Sikushangaa kwa sababu ninawajua ni watu wenye tamaa na kuendekeza njaa njaa zisizo na msingi.

Ila wahusika ni vyema mliangalie hili. Nafkiri hao watumishi wenu wanahitaji vetting ya kutosha kuwa hapo.
 
Back
Top Bottom