GE2025 Suphian Juma achukua fomu CCM ya kutia nia Ubunge jimbo la Ikungi Magharibi

GE2025 Suphian Juma achukua fomu CCM ya kutia nia Ubunge jimbo la Ikungi Magharibi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
2,186
Reaction score
4,940
Mimi ndugu Suphian Juma Nkuwi, kada mtiifu wa chama cha Mapinduzi,CCM na Mkurugenzi wa Shirika la TAA linaloratibu kampeni ya kupanda miti mkoa mzima wa Singida iitwayo SINGIDA MPYA YA KIJANI INAWEZEKANA leo Julai 01, 2025 nimechukua na kurejesha fomu kugombea nafasi ya Ubunge jimbo la Ikungi Magharibi.

Nimechukua maamuzi haya adhimu nikitambua kwamba jimbo letu la Ikungi Magharibi lina kiu kubwa ya Mbunge mpya na sahihi atakayeoana na kasi, utashi na siasa safi za Mhe. Rais Dkt Samia.

Aidha naamini kwamba mimi nikishirikiana na wana ikungi wenzangu tutaleta mageuzi makubwa na chanya kwenye maadili ya uongozi, Haki za Binadamu, Uongozi shirikishi, Demokrasia, Umoja na Upendo baina ya makundi yote bila kibaguana ambavyo vyote hivi kwa pamoja vitachagiza ukuaji wa uchumi wa kila mwananchi mmoja mmoja.
SUPHIAN JUMA NKUWI; Jimbo jipya, Mbunge mpya na maendeleo mapya.

MWAJIFYA INO ANYANKUNGI UMWEI
‼️

Suphian Juma Nkuwi,

1751377598446.png
 
Mwenzako elibariki katandaza mabango yake puma, ikungi na sepuka ina maana ana uhakika wa kurudi bungeni. Sasa ukimshinda huoni kuwa atang'oa mabango yake na we kulazimika kusimika mapya? Umedhamiria kugombea kwa dhati au unamsindikiza elibariki tu? Halafu hilo si jimbo jipya mjuba, sema ni jina jipya, zamani jimbo hilo liliitwa singida magharibi
 
Back
Top Bottom