Ndimbo M
Member
- Aug 30, 2023
- 13
- 62
Wakati serikali imesema inaingia hatua ya pili ya mkataba katika uwekezaji bandarini Dar kati yake na DP world,ningependa watu wote bila kujali kama mnaunga mkono au kupinga maudhui ya mkataba, msome kwa umakini haya nitakayoyaandika hapa chini, mpime katika mizani ya bongo zenu,kisha mseme tunafanyaje au mnawashauri nini hao watakoingia mezani na DP kuwakilisha maslahi ya Tanzania.
DP world iliingia mkataba wa miaka 30 na Djibouti mwaka 2006 wa kuendesha sehemu ya container terminal katika bandari ya Doraleh. Katika shughuli ya uendeshaji wa kitengo cha makontena katika bandari hiyo ya Doraleh, DP world walikuwa na hisa ya asilimia 33.,kampuni ya China Merchant ya Hong Kong ina 25% ,na hisa zinazobaki ni za kampuni ya SDGT inayomilikiwa na serikali.
Kuanzia mwaka 2011,Djibouti ikaanza kuiomba serikali ya UAE kwamba wakae tena mezani ili kujadili upya vipengele vya mkataba kati yake na DP world kwa vile kwa hali ilivyo,vipengele vya sasa siyo vya haki na vinabana maslahi ya Djibouti. Serikali ya UAE ikakataa kabisa. Vipengele vya mkataba kati ya Djibouti na China Merchant vina maslahi kwa Djibouti.
Lakini hapo katikati,mwaka 2016 kukatokea jambo jingine kubwa. DP world ikatangaza itajenga Free economic and special zone katika eneo la Somaliland huku tayari wakiwa wameshaingia mkataba na Somaliland wa kuendesha bandari yake ya Berbera katika mkataba wa miaka 30.
Baada ya hilo tukio,Dp world wakaanza kuwashawishi Ethiopia kwamba waache kutumia bandari ya Doraleh, Djibouti..badala yake watumie bandari ya Berbera ambako kutakuwa na malipo ya chini sana kwa sababu ya hiyo Economic free zone anayoijenga pale. Djibouti haikupendezwa na hicho kitendo cha DP hasa ikichukuliwa kwamba asilimia 95 ya mizigo yote ya Ethiopia inapitia Doraleh port, na hivyo ikaamua kuchukua hatua.
Hatua iliyochukuliwa na Djibouti ni kuvunja mkataba na DP na kuwaondoa, hivyo shughuli zake kuchukuliwa na DSGT,kampuni ya serikali pamoja na China Merchant.
DP walishtaki mahakama ya kimataifa na kesi kuamuliwa kwamba DP inatakiwa kulipwa fidia ya dollar 486 milioni,na pia irejeshwe katika sehemu yake ya kazi kulingana na matakwa ya mkataba. Djibouti imegoma kutekeleza maamuzi ya mahakama, japo mahakamani ilijitetea na kushindwa kuthibithisha kwamba DP world waliingia mkataba na Djibouti kwa hila,kwa kumhonga aliyekuwa mtendaji mkuu wa mamlaka ya bandari bwana Abdourahman Boreh,ambaye alikimbia nchi baada ya muda mfupi.
Sasa turudi katika mandhari na muktadha kati ya Tanzania na DP world.
Serikali kupitia watendaji wake wamerudia kusema kwamba ni muhimu kuingia mkataba na DP kwa kwa lengo la kuongeza ufanisi na tija, huku wakitaja kiasi kikubwa cha mapato kitakachoifanya Dar port kuwa na mchango mkubwa katika pato la taifa,GDP, japo hatujui hadi sasa kwamba mgawanyo utakuwaje kati ya DP na serikali.
Watendaji wa serikali tumewasikia pia wakisema wameichagua DP kutokana na uzoefu wao katika shughuli za uchukuzi na wingi wa wateja ilionao.
Lakini kitu ambacho hawajasema kwa wananchi au hawajajiuliza ni ukweli kwamba DP world ni kampuni inayojiendesha kibiashara kwa kufurahisha wateja wake, na katika kutimiza azma hiyo itafanya lolote hata ikiwa uamuzi wake utamuumiza mshirika/mwanahisa mwenza katika kazi kama ilivyotokea kwa Djibouti.
DP ikishapata kibali cha kufanya kazi katika bandari za Mombasa na Dar, Kenya itafanya nini au imejipangaje endapo DP atashawishi wateja wa Mombasa port kupitisha mizigo yao Dar port?
Tanzania imejipanga vipi endapo DP ataanza kazi Beira,Mozambique na kuwashawishi wateja wazoefu wa Dar port wa nchi za Congo, Rwanda, Burundi, Malawi na Zambia kupitisha kazi zao Beira baada ya DP kupima faida yake? Na hilo ni rahisi tu kutokea ukizingatia umbali toka Beira port hadi Blantyre, Malawi ni kilomita 689 tu,ukilinganisha na Dar hadi Blantyre, kilomita 1800. Pia umbali wa Dar-Lusaka ni km 1948, wakati umbali wa Beira-Lusaka ni km 1056 tu.
Lakini ninaposema ikiwa DP atapima faida atakayopata katika kuwawahishia wateja wake mizigo kwa kutumia vigezo vya umbali na namna alivyoingia mkataba na bandari husika. Tuchukulie mathalan, mkataba baina ya DP na Dar port,unaipa maslahi makubwa Tanzania,lakini DP ikafanikiwa kuingia mkataba wa faida kubwa kwake kati yake na Beira port, ni wazi kwamba atahakikisha anahamisha wateja wake toka Dar na kuwapeleka Beira.
Kimsingi UAE hawafichi jambo moja, kupitia DP world wanataka kupata umiliki wa kuendesha bandari zote za pwani ya Afrika hasa upande huu wa bahari ya Hindi kuanzia Djibouti, Somaliland, Somalia, Kenya,Tanzania na South Africa ili kwanza kujipatia faida kwa kurahisisha biashara zake za uchukuzi, na vilevile kuziangalia kwa ukaribu hizo bandari zisije kuwa mshindani wake wa karibu na kuhatarisha maslahi ya bandari yake ya Jebel Ali, Dubai.
Binafsi, naona hatua ya kwanza ya kuchukua ni kuibana DP ili Tanzania iwe na maslahi makubwa katika mgawanyo wa mapato.
Pili, Tanzania lazima ihakikishe inaibana DP ili iweke bayana ni namna gani itakuza pato la Dar port kama inavyojinadi kuwa ina uwingi na mlolongo wa wateja ilionao sasa na hata wateja inaotarajia kuwaongeza pindi ikianza kazi; na katika hilo Tanzania inatakiwa kuifunga DP kwa kipengele kwamba wateja wote walioko katika nchi zinazotuzunguka, ni lazima watumie Dar port; na kwamba kwenda kinyume na hilo itachukuliwa kama ni kitendo cha kuvunja mkataba.
Tatu, kama DP haitaridhia vipengele nilivyovitaja hapo juu, Tanzania ni lazima iachane na mwekezaji wa namna hiyo. Hapa sijataja vile vipengele ambavyo vimepigiwa kelele na watu wengi ambavyo havistahili hata kuwepo na kujadiliwa, kama kile cha kuitaarifu kwanza UAE endapo Tanzania inataka kuendeleza bandari nyingine, mathalan,Tanzania ikiazimia kuiendeleza Bagamoyo port sambamba na special economic zone yake kwa kiwango kilichotajwa mradi ambao utakuwa tishio kwa bandari ya Jebel Ali, Dubai.
Kwahiyo tutarajie wakubali?