Surprise visits.....

Surprise visits.....

Dr Lizzy

Platinum Member
Joined
May 25, 2009
Posts
31,009
Reaction score
60,629
Good morning/good afternoon/good evening/ good night to y‘all!!

Nimekumbuka kuna kaka mmoja alikua mpenzi wa mtu wangu wa karibu yani sijawahi ona mtu ‘CONTROLLING‘ kama yule.Alikua anawasiliana na mdada kujua yuko wapi kila saa...unakuta mdada anamjibu “nipo kazini bado....utatoka saa ngapi?!...soon....then unaenda wapi?!....straight nyumbani!!...ohhh owkey tutaongea basi baadae ukifika mpenzi!

Wanaagana dada anamaliza shuguli zake huyooo nyumbani.Akifika either anaweza kumkuta mshkaji anamsubiria nje kwake au baada ya kama dakika tano hivi anakuja...unakuta alikua amekaa jirani akimwangalia.Nia kuu ya hizi ‘SURPRISE VISITS“ alizokua anafanya ilikua kuhakikisha hadanganywi ila sasa mimi nataka kuongelea zile zinazofanywa kumsurprise mume/mke/mpenzi ambae amekumiss nawe kummiss.Either kwasababu kila mmoja anaishi kwake...safari za kikazi/kimasomo au mnaishi mikoa/nchi tofauti.

Je wewe una/ungefurahia kama mwenzako akikushangaza kwa ujio wake?!Bila wewe kutarajia ila uwe na hamu ya kua nae karibu ndo nnayoongelea...sio ile ya mwenzio akisafiri unasema “AHHHH ASANTE MUNGU“.Personally napenda sana...unakuta mtu hata kama ni uchovu unaisha...hasira zinapotea...upweke unakimbia...n.k

Na vipi kumshangaza wewe??Hii pia naona ni nzuri pia ila inapaswa uwe umetumia akili kujua ukimshtukiza mwenzako ataREACT vipi usije ishia kuulizwa “unafanya nini hapa?“ kama ni kwake au “mbona umewahi sana kurudi?!“ kama ni kwenu huku mtu sura amekunja...kwa maana nyingine asiyefurahia uwepo wako bila kumpa ‘heads up‘.
 
Surprise visits si jambo baya kama ikifanywa mara chache sana..mfano umesafiri na pia ukiwa umetoa taarifa mapema.. yaani unaweza sema..unitegemee J3, J4 au J5..hapo mwingine anajitaharisha kimawazo..na hamu inapanda.. Lakini hii mipango ya kufanya surprise visits kama unawinda kufumania na ku-control ni mbaya sana ..kwani zinaweza sababisha kutoaminina na ni dalili za shari...

Mimi binanfsi sizipendi.. na niko muwazi..sitaki na sitafurahia..
 
kwakweli ni afadhali umjulishe kua natarajia kuja wakati wowote manake duh unamkuta mtu kavimbisha mdomo kama alotiwa Hamira,baada ya kufurahi,au unamkuta hayupo....
 
kwakweli ni afadhali umjulishe kua natarajia kuja wakati wowote manake duh unamkuta mtu kavimbisha mdomo kama alotiwa Hamira,baada ya kufurahi,au unamkuta hayupo....
Hahhaha...eti kavimbisha mdomo kama katiwa amira...well ndo maana ni muhimu kujua yeye analichukuliaje hilo swala.TULIZO....uloyosema ni kweli...inapendeza tu pale inapofanyika kwa nia nzuri na wote wakafurahia.
 
Lizzy hizi ni nzuri but isiwe too much kwa sababu itafika wakati mwenzio ataanza kuzitafsiri vinginevyo: Humuamini, wivu n.k tafsiri ambazo zitamfanya asifurahie tena ujio wako.

Ila pia inategemea na usafi wa mtu (Hana vimeo lol) kama ni msafi mydia kwake atafurahi but kama ndo ana-vi'shughulisho' vingine utakuwa unamzibia.

Nilisawahifanya moja, nikapata nilichopata na nikaapa kutorudia tena!!
 
Ni bora kumfahamisha kuwa unaweza kuja wakati wowote at least by saying that anaweza kufurahia zaidi maana wengine wakifanyiwa SUPRISE VISIT kitu kitakochomujia kichwani cha kwanza ni kuwa either unataka kumfumania or something else.
 
bora awaze tu kuliko afumaniwe kweli! surprise visit ni nzuri kwa mahusiano stable yasiyo na shaka!kama unampenda mwenzio,mnashirikishana mipango,mafanikio na failures zenu anakuwa anajua what is up with u.so any surprise visit inakuwa nzuri na kwa kweli kama ni uchovu ama huzuni inatoweshwa.ila kama ndo ana mambo yake,lazma midomo iumuke!na huo ni ujumbe tosha!mwenye macho haambiwi tazama!
 
Msiangalie vitu upande mmoja,lets say mnaishi mikoa tofauti labda kama ni bongo MWZ-DAR ukajifanya unajua masurprise visiti umetoka MWZ unaenda dar,umefika Singida gari likaharibika ukagundua matengenezo yake yatakulazimu ulale mara umekutana na mtu anakufahamu akampigia mpenzi wako na kumwuliza,hivi mehamia singida siku hizi?mbona nimemuona mume/mke wako hapa?unategemea nini kitafuata hapo nia yako inaweza kueleweka vizuri kweli?

Unajua unaweza ukawa na nia nzuri but usifikie lengo?

 
mmmmh hayo ma-suprise visit mie hata siyataki, kuna rafiki yangu wa karibu na mwenza wake walikua mikoa tofauti, akaamua kumsuprise akaishia kujisuprise mwenyewe baada ya kufumania live, kisa cha ugonjwa wa moyo maisha yenyewe mafupi, heri nitoe taarifa, ingawa hili pia linategemea tabia za mwenza wako, ujijua anapenda suruali/sketi bora umwambie kua waenda

jambo jingine barabarani kuna mengi jamani, kama mikoa tofauti mweleze ila kama mko mkoa mmoja na unaamini una kifua msuprise tu...
 
Akinifanyia suprise visits zaidi ya 3 namwambia yaishe bwana..mana huko ni kuchungana kuliko pitiliza hivyo hana imani nami basi hamna haja ya kuwa pamoja..Nia ya hizi 'suprises' haziwagi nzuri ndiyo maana sizifagilii..!!
 
Ahahaha...yani hamtaki kabisa?!Kwanini mnahisi lazima mtu awe anafanya kwa ubaya (kukuchunguza..kutokukuamini) na mengineyo kama hayo?!

BE umeniacha stendi ya Ubungo...uendawazimu unatoka wapi hapa?!

MJ...asante kwa kaeksipiriensi mpendwa...wakati mwingine unakutana na usiyotarajia ila muhimu kujua...sio mwenyewe wajiaminisha ni wewe tu kumbe kuna wenzako watatu...bpra kujua na kuamua kama UNAKUBALI au UNAKATAA mapungufu ya mwenzako.
 
suprise ziwe na kiwango...zikizidi inakuwa kero na maana yake inatoweka na kuwa jaribio la fumanizi.
 
Nasema hivii:

Kama bibi yenu anapenda awe surprised basi anifanyie surprise visit..........

Surprise Visits ni ugonjwa wa wivu uliopitiliza. Yaani ni kama ukichaa flani hivi.
 
Nasema hivii:Kama bibi yenu anapenda awe surprised basi anifanyie surprise visit..........Surprise Visits ni ugonjwa wa wivu uliopitiliza. Yaani ni kama ukichaa flani hivi.
Loh....kazi mbona anayo bibi wa watu.Na kweli asijaribu asije akafa kwa presha siku sio zake!
 
Back
Top Bottom