GE2025 Suzan Kiwanga: CCM ni sawa na manyani, 2025 ama zao ama zetu, nyani hasusiwi shamba la mahindi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Matangini, Mlimba – Morogoro, Suzan Kiwanga alisisitiza kuwa haoni sababu ya chama tawala kuachwa kipite bila kupingwa, akisisitiza kuwa wapinzani hawapaswi kususia uchaguzi bali kupambana hadi mwisho – mvua au jua.

Kwa mujibu wake, kama kuna gharama ya kupambana kisiasa, basi bora ipatikane kupitia sanduku la kura badala ya vurugu au migogoro isiyo na tija.

Namnukuu,

"Mimi nimesema hivi 2025 ama zao, ama zetu nyani hasusiwi shamba la mahindi, utaenda kuvuna mabua kwahiyo dawa yao CCM ni kupambana nao iwe Mvua iwe jua, mpaka kieleweke. Mimi simuogopi CCM wala baba yake CCM, bampa kwa bampa mpaka kieleweke, bora nifie kwenye boksi la kura kuliko nife wakati naenda kuzuia uchaguzi.

Sasa watu wazima tunadanganywa ooh tukazuie uchaguzi, nikawaangaliaa nikasema hivi ninyi mnatuona wote matahira eenh, hivi sisi tuna ubavu wa kuzuia uchaguzi? Kile Chama nilichokuwa wamekataa kuingia kwenye uchaguzi, Tukikiacha Chama Cha Mapinduzi kipite bila kupingwa, tutakuwa na mapungufu ya akili. Nawaambia mama Kiwanga ni yuleyule wala hajabadilika na CCM wananitamani na mimi sitaki CCM na ndiyo maana nimekuja CHAUMMA ili tupambanie maendeleo yetu wana Mlimba, CCM hawana jipya."

Safi kabisa
 
Back
Top Bottom