Tuanze na history kidogo. Hiyo gari (Grand Escudo) ni kichipukizi cha Suzuki Escudo hizi za kawaida.
Suzuki Escudo ndio hiyo hiyo Suzuki Vitara, kwa kuongeza msisitizo zaidi.
Tukianza na izo Vitara/Escudo, zipo generations kadhaa nadhani wewe ulioiweka kwenye picha ni 2nd generation, ambayo ni mwaka 1999 hadi 2005 hivi sasa sijui exactly mwaka gani unataka.
Pia kwa issue ya wese zinakuja na engine size na model tofauti tofauti kuanzia ndogo 1.6L i4, 2.0L i4 na kubwa 2.5L i6 engines, zote Petroleum za Diese zipo ila nadra. Ila engines ni tofauti tofauti lakini reliability zipo vizuri.
Hiyo Grand Escudo ni ndefu zaidi na ina nguvu zaidi kuliko Escudo za kawaida. Wanaiita Suzuki XL-7 jina jingine.
Demu mmoja kazini anayo. Aisee inaunguruma ile gari hatari, ila uwa analalamika mafuta ulaji wake upo juu, approximately 8km/L on average, hapa mjini Daslam.
Sasa hio XL-7 yenyewe ina generation mbili tu, iyo ulioiweka wewe ni 1st gen. Usichanganye madesa. 1st gen ya hii XL-7 ina share vitu vingi na 2nd gen ya normal Escudo. Tuseme hivo.
Hii engine kubwa kiasi maana ina flavor ya 2.5L V6 na 2.8L V6, zote petrol za Diesel mi sizikumbuki sana.
Ukiwa fresh, tafuta la 2004/2005 hivi haya yalifanyiwa facelift kwahiyo yana modification za muonekano na performance kiasi.
Turudi kwenye swali.
Kama wese kwako issue achana nalo. Ila spare na reliability, Suzuki wako vizuri.