Habarini wadau kutokana na shughuli zangu za hapa na pale. Nahitaji kununua Pikipiki Aina ya Suzuki Tf125 mwenye uzoefu nayo au anayewahi kutumia. Na je? Dukani inafika kiasi Gani kwa sasa,
Uimara
Ulaji mafuta
Hiyo ni two strock, ukisahau kuweka tu inakaanga injini, unaenda kuchonga block yake, na mwisho kuchonga ni mara3 , na kadiri unavyoongeza ukubwa wa piston ndio ilaji wa mafuta unaongezeka na power pia.
Haifai achana nayo inahitaji umakin sana
Hizo pikipiki nimeendesha kwa miaka 3. Ni nzuri sana tatizo lake ni
1. moshi mwingi sana maana inatumia two stroke (moshi ukikata jua unakaanga engine soon).
2. Spea zake kupata ni balaa kubwa mno na ziko expensive
3. Inakula mafuta kwa fujo
4. Gharama ya kuinunua iko juu na siku ukiamua kuiuza hutapata mteja. Au ndo utaiuza kwa bei ya fekon
HITIMISHO
Tafuta pikipiki ya kawaida tu. Hizi waachie serikali na DFP ndo wanazimudu.