Suzuki Tf125

Suzuki Tf125

Genious862

Member
Joined
Aug 15, 2018
Posts
78
Reaction score
21
Habarini wadau kutokana na shughuli zangu za hapa na pale. Nahitaji kununua Pikipiki Aina ya Suzuki Tf125 mwenye uzoefu nayo au anayewahi kutumia. Na je? Dukani inafika kiasi Gani kwa sasa,
Uimara
Ulaji mafuta

Karibuni wadau
IMG_20180902_210648_281.JPG


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo pikipiki ina fuka moshi mweupe balaa,sikushauri kabisa.
Zingatia ushauri wa wadau kuhusu pikipiki za kichina
 
Hiyo ni two strock, ukisahau kuweka tu inakaanga injini, unaenda kuchonga block yake, na mwisho kuchonga ni mara3 , na kadiri unavyoongeza ukubwa wa piston ndio ilaji wa mafuta unaongezeka na power pia.
Haifai achana nayo inahitaji umakin sana
 
Bei yake itakua simchezo sawa na gari ndogo.plus mlio wa ovyo sana
 
Hizo pikipiki nimeendesha kwa miaka 3. Ni nzuri sana tatizo lake ni
1. moshi mwingi sana maana inatumia two stroke (moshi ukikata jua unakaanga engine soon).
2. Spea zake kupata ni balaa kubwa mno na ziko expensive
3. Inakula mafuta kwa fujo
4. Gharama ya kuinunua iko juu na siku ukiamua kuiuza hutapata mteja. Au ndo utaiuza kwa bei ya fekon

HITIMISHO
Tafuta pikipiki ya kawaida tu. Hizi waachie serikali na DFP ndo wanazimudu.
 
Back
Top Bottom