Swabrina Ghalibu, Msichana wa kwanza Mdogo kufanya kazi Mortuary

Swabrina Ghalibu, Msichana wa kwanza Mdogo kufanya kazi Mortuary

Anaitwa Swabrina Ghalibu huyu atakuwa ni msichana wa kwanza kabisa kufanya kazi Mortuary akiwa na Umri mdogo ana Miaka 19

Atakuwa anatunza miili ya binadamu Mortuary na kuifanyia kila Taratibu zote.....Wakati akina dada wengine waki jimwaya mwaya Instagram na Facebook huku hawana Kazi yeye atakuwa anafanya kazi hiyo ambayo itakuwa inamuingizia pesa Nzuri tuu

Ni kazi ambayo haina ushindani hivyo ukiomba ni rahisi kupata

Kwa nijuavyo mimi kazi ya huyo dogo itakuwa kukusanya miili hiyo toka mawodini,ICU,na sehemu zingine za hospital na kuipeleka Mortuary,atakuwa anaisafisha kwa kuogesha miili hiyo,kuwatolea watu miili yao wanapo kuja kuichukua!

Haya sasa Ni wakati wa kina dada wengine kujifunza
93033faa983b488b31abf8019fb6047a.jpg
wako wenye 14tunapiga kazi njoo uswaz
 
Asije kuwa mchawi, na yuko pale kimkakati. Maana hiyo kazi huwezi niambia ilikuwa ndoto yake nikakuelewa.
 
Asije kuwa mchawi, na yuko pale kimkakati. Maana hiyo kazi huwezi niambia ilikuwa ndoto yake nikakuelewa.
Kwa nini uhisi hivyo? Wakati mwingine si ndoto, unajikuta tu unapenda kazi flani au unataka kazi fulani. Pengine si kwa sababu ya ndoto ila maslahi. Na wengi inawatokea.

Mimi nawaheshimu sana hawa Watu, wakati ndugu mnakaa mbali mkiogopa maiti yenu, yeye anamhifadhi na kumuosha.

Kuna mmoja nilimwona Sekou Toure Hospital Mwanza anaijua hasa kazi, yuko smart na hakuna harufu yeyote mbaya utakayoisikia. Kwa mara ya kwanza nilikaa mortuary kwa muda mrefu tena comfortably wakati anamuosha na kumuandaa ndugu yangu
 
Hivi package ya kada hii kwa mwezi huwa ni kiasi gani - kwa rate za kiserikali
 
Mara nyingi hawa mortuary attendants na undertakers wanakuwaga machizi fulani hivi kichwani, dah, kucheza na maiti zingine zilipata ajali zinakuja jicho moja hamna sura imevunjika, hapana! NGOJA NIENDELEE TU KUWA MWANAUME WA DAR.
 
Huyo dada jasiri. Acha niendelee kusaka ajira ila hiyo kazi inahitaji moyo wa ziada.
 
Watanzania bwana!! Kwani huyo binti kachukuliwa tu mtaani na kupelekwa hapo mortuary.

Mie nafikiri ameshapata mafunzo maalumu ya hiyo kazi
Ni sawa na 1st year wa MD wanaposoma course ya Anatomy na yale makadava(maiti za kujifunzia) lazima uandaliwe kisaikolojia ,mie namjua mtu ambaye alikuwa muoga lakini now he is a good doctor na anadili na maiti kila siku
 
Tumbi hahahahaha
Hewallah mambo si hayo huwa tunahitaji mwanzo khalafu mwisho utajulikana ukipita bint jasiri kama huyo unafarijika sio hawa wa kuogopa mende akiingia ndani kinabana pua"baby kuna bonge la mdudu ndani"
 
Kwa nini uhisi hivyo? Wakati mwingine si ndoto, unajikuta tu unapenda kazi flani au unataka kazi fulani. Pengine si kwa sababu ya ndoto ila maslahi. Na wengi inawatokea.

Mimi nawaheshimu sana hawa Watu, wakati ndugu mnakaa mbali mkiogopa maiti yenu, yeye anamhifadhi na kumuosha.

Kuna mmoja nilimwona Sekou Toure Hospital Mwanza anaijua hasa kazi, yuko smart na hakuna harufu yeyote mbaya utakayoisikia. Kwa mara ya kwanza nilikaa mortuary kwa muda mrefu tena comfortably wakati anamuosha na kumuandaa ndugu yangu
Nilimaanisha kazi ya ndoto yake. Mdogo wangu dunia imeharibika mno na kuna kila aina ya watu. So uwezekano wa kuwa mchawi upo, sisemi ni mkubwa lkn upo. Hard to swallow ktk umri huo unapata ujasiri wa kufanya kazi hiyo. Wanaofanya kwa moyo, nawapongeza maana wanatuhifadhia ndugu zetu na watatuhifadhi tukibaatika kufa na miili yetu ikaonekana.
 
Binti mdogo sana, kazi kubwa sana anayofanya haendani nayo. Mungu amlinde kwa kazi hiyo.
 
Duh... hayo ni matumizi mabaya ya rasilimali watu!! ina maana binti mrembo mbichi mbichi kama huyo hatujaona kazi nyingine ya kumpangia mpaka tumuweke mortuary.....

Hili jipu inabidi litumbuliwe mapema... aliyehusika kutoa ajira na wenzake wote watumbuliwe....
 
Back
Top Bottom