Swahiba ampa mimba mtoto wa rafikie ambaye ni denti kidato cha 4

Mkuu hivi vitu vigumu sana.....! Hiyo miaka ni mathematics tu sio biological bana! Sie tunalazimisha vitu tu ilimradi. Basi ingelikuwa hakuna msichana/mvulana kubalehe mpaka afikishe miaka hiyo, lakini mambo sio hivyo.
 

Mkuu BornTown
Ishu nimeisoma na inasikitisha sana kwa yote yaliyotokea. Binafsi bado nasimama pale pale kama ingekuwa ni mie ndo mzazi, swala hili lingefika polisi. Kuna mkondo wa watu wengi watausika, pale shuleni inawezekana kuwa walivuta mshiko. Ukipeleka mtoto wako shule unakuwa na imani na walimu waliopo kuwa watasimamia malezi ya mtoto wako kwa umakini na-kwa uwezo na taaluma yao inavyowaelekeza. Sasa kushindwa kuchukua hatua yoyote ya kumfahamisha mzazi mapema binafsi haingii akilini zaidi ya kutaka kuona wote waliohusika wanafika kwenye vyombo vya sheria. Chukua hatua leo kupunguza huu ubazazi. Ifike pahala watu wawajibike kutokana na matendo yao, ingekuwa Uchina hapa tungekuwa tunaongelea kesi ya kunyongwa, Sheria zao ni kali ata mtu akitaka kufanya kosa anajiuliza mara mbili mbili. Kwa hii ishu sheria zetu zipo wazi, potelea mbali kama ni uswahiba ufe lakini sio kuendekeza unafiki. Poleni wakuu.
 
Wanajamvi ninashukuru sana kwa michangao yenu, hivi niandikavyo mama wa binti ametinga police ili sheria ifuate mkondo wake, nitawataarifu yale yatakayoendelea.
 
Kimsingi kwa mtu yeyote mwenye hekima, mwenye adabu na mstaarabu, watoto wa rafiki yake wa kufa na kuzikana ambao tena bado ni wanafunzi ni sawa na watoto wake wa kuzaa. Huyo hakuwa na urafiki wa kweli bali alikuwa ni partner tu wa kibiashara kitu kilichompa nafasi ya kuwa karibu na watoto(inawezekana hata mke) wa mwenzake na kupata urahisi wa kuwarubuni na kuwachezea bila kushitukiwa upesi. Huyu bazazi kama ameweza kumfanyia hivi rafiki yake basi uje amewaharibia mabinti wengi sana. Huyu anasitahili adhabu kali sana kutoka vyombo vya dola.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…