Swahili Programming Language - swap

Swahili Programming Language - swap

abdulbasit

Member
Joined
Oct 30, 2018
Posts
7
Reaction score
19
Swahili programming language (swap) ni lugha ya kuprogram kwa kutumia maneno ya Kiswahili, ni lugha ya kwanza kabisa kuruhusu mtu kuweza kuandika kodi kwa kutumia maneno ya kiswahili (swahili lexical terms), lugha hii ilizinduliwa rasmi tar 2020-05-24 , lengo kuu ikiwa ni kusaidia kujifunza kuprogram kwa kutumia kiswahili.

Lugha hii imetengezwa juu ya nodejs ambao ni mfumo (frame-work) uliotengezwa kupitia JScript, kwa kifupi tunasema kuwa lugha hii imetengenezwa na Jscript.

Code:
hifadhi jina = dai("unaitwa nani: ");
andika "karibu "+jina+;
andika "
1. saizi yako
2. siku + Bonas
3. wiki + Bonas
4. halichachi
";
hifadhi chaguo = dai("weka chaguo lako: ");
wakati(chaguo > 0){
    chagua (chaguo){
        kesi 1:
            andika "umejiunga kifurushi cha saizi yako";
            vunja;
        kesi 2:
            andika "umejiunga kifurushi cha siku";
            vunja;
        kesi 3:
            andika "umejiunga kifurushi cha wiki";
            vunja;
        kesi 4:
            andika "tumia kifurushi chako bila kikomo";
            vunja;
        zaidi:
            hifadhi chaguo = dai("umekosea weka chaguo lako tena: ");
    }
}

Huo ni mfano wa programu fupi ya uchaguzi wa vifurushi kutumia lugha ya swap ambao kama tukiendesha programu hiyo tunapata matokeo yafuatayo

Code:
unaitwa nani: abdulbasit
karibu abdulbasit

1. saizi yako
2. siku + Bonas
3. wiki + Bonas
4. halichachi

weka chaguo lako: 7
umekosea weka chaguo lako tena: 8
umekosea weka chaguo lako tena: 7
umekosea weka chaguo lako tena: 4
tumia kifurushi chako bila kikomo

programu hiyo kama tungeiandika kwa lugha ya C++ basi ingekua katika mfumo ufuatao

C++:
#include <iostream>
#include <string>
using namespace std;

int main(){
    string jina;
    int chaguo;
  
    cout<<"unaitwa nani";
    cin>>jina;
    cout<<endl;
  
    cout<<"karibu "<<jina<<endl<<endl;
    cout<<"1. saizi yako"<<endl
        <<"2. siku + Bonas"<<endl
        <<"3. wiki + Bonas"<<endl
        <<"4. halichachi"<<endl;
  
    cout<<"weka chaguo lako: ";
    cin>>chaguo;
  
    while(chaguo>0){
        switch(chaguo){
            case 1:
                cout<<"umechagua kifurushi cha saizi yako"<<endl;
            ...
                default:
                    cout<<"umekosea weka chaguo lako tena: ";
                    cin>>chaguo;cout<<endl;
        }
    }
}

Namna ya kuipata swap
github : ibnsultan/swahili-programming-language
nodejs: swapro

Usisite kuandika maoni yako na kutuchangia ili kuendeza kazi hii na kama kuna makosa basi ni ubinadamu, kwani hakuna mkamilifu
 
Swap ni JavaScript framework?? Ni scripting language?? Inherited from JavaScript????
 
Umejitahidi mkuu lakini kama kawaida hutapata mtu humu watu wanawaza betting na easy money nyinginezo
 
Hii ni mwanzo mzuri sana. Ila mm mawazo yangu ni kwamba kipatikane kitabu cha kiada cha kiswahili ktk shule za awali( hasa za umma) chenye namna murua ya kuwavuta watoto kujua umuhimu wa lugha za kuprogramia. Then tutafika kwenye hizi vitu za kujenga juu ya framework kama hizi.
 
Bora kiingereza tu Hichi kiswahili ni kigumu mno
 
Swap ni JavaScript framework?? Ni scripting language?? Inherited from JavaScript????
hapana, swap ni lugha inayojitegemea, lakini interpreter yake imetengezwa kwa javascript, kama ilivyo python kuwa ni lugha inayojitegemea lakini interpreter yake imeandikwa kwa C.
Ijapokua kwa sasa swap ni lugha changa, na programing yake inafanika kwa CLI interface pekee.
 
Mkuu usisikilize hawa baadhi ya hopeless africans wao wanaamini chochote hakiwezekani that's why wanachojua ni kuponda tu wakishakaririshwa ili wapate ajira.

Good work mkuu naendelea kukufuatilia africa inahitaji watu kama wewe.
 
safi sana mko vizur tunategemea zaidi kutok kwenu
Industry ya programming inahitaj watu kama ninyi hasa bongo ambapo bado kuna uhaba wa practical programmer
 
Hongera sana mkuu. Hii ni bonge la project, kiukweli itawasaidia watu wanaoanza kwa programming kupata zile concept za mwanzo kwa lugha inayoeleweka
 
Back
Top Bottom