Jamani kama kichwa cha habari kinavyojieleza nimekaa na kutafakari kuhusu mnyukano unaoendelea kuwahusu hawa wabunge al-maarufu covid-19. Ikiwa uchaguzi wa 2020 uliolalamikiwa na chadema na watanzania wengi kwamba haukuwa wa haki na kupelekea zaidi ya 99% ya wabunge wa ccm kuteuliwa na katika mwendelezo huo huo wakapatikana wabunge 19 wa covid-19.
Hivyo sioni mantiki yoyote ya chadema kukomaa na hawa 19 na kuwaacha wale 99% ambao nao waliingia kimizengwe. Ningeshauri wapiganie zaidi kupata mfumo ambao utaweka mazingira yatakayopelekea uchaguzi huru na wa haki ambao utaafikiwa na vyama vyote na wadau wengine wa uchaguzi...