Swala la kumpeleka Musonda Mazembe watupe Baleke, tutaumia

Swala la kumpeleka Musonda Mazembe watupe Baleke, tutaumia

Its Pancho

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2018
Posts
15,966
Reaction score
26,404
Wakuu

Nimeskia sana tetesi kuwa kutakuwa na swap deal kati ya Yanga na Mazembe

Means Musonda kwenda Congo na Baleke aje Yanga.

Huu usajiri kwa kweli tunaenda kupigwa kama kweli, pakubwa sana. Why?

Mpaka Mazembe wanakuja kwako kumtaka mchezaji ujue huyo ni a good player! Halafu pia hawa ni washindani wetu means tunaweza kukutana nao huko CAF

Huyu Baleke kama mzuri sana mbona wao hawamtaki wanaishia kumtoa kwa mkopo hovyo?

Simba karibu two seasons na Libya huko why?

Halafu tuwape Musonda kirahisi sana?

Tukumbuke kuwa tangu Musonda hajaja Zambia jamaa walikuwa wanamtaka sana ni vile Yanga waliwazidi kete Mazembe ..

Injinia huu usajiri achana nao nimeona Baleke yupo Dar tayari bora aende Simba au Azam huko.

Dube anatosha sana kwetu sio huyo Baleke ..

Unaweza kupinga pia.

Nawasilisha wakuu
 
Than Dube?

Jamaa ni hatari sana huyu mzimbabwe sema majeraha
Akija yanga atakutana na doctor yousoph pale mbona atakaa sawa mtakubali mziki wake wakuu
Dah nasikitika kusema Yousoph hatuko nae msimu ujao jamaa karudi tunis
 
Kwani Yanga inahitaji Washambuliaji wangapi? Dube au Baleke?

Dube ni mzuri kuliko Baleke na Baleke ni mzuri kuliko Musonda. Ni vyema zaidi kama tukamsajili Dube na tufaye swap ya Kinzumbi kwa Musonda.
 
Sidhani kama Baleke yupo Tanzania kwaajili ya Yanga hasa ukizingatia kuna tetesi za kubakia kwa Guede na kuongezeka kwa Dube. Maanake eneo la ushambuliaji tayari litakuwa wamelimaliza itabakia maeneo mengineo na pia itabakia nafasi finyu sana kwa wachezaji wapya wa kigeni hivyo ni lazima kupunguza mchezaji ili aingie mchezaji. Naona Skudu, Okrah na Lomalisa huenda wakawa sio sehemu ya kikosi cha Yanga msimu ujao.
 
F nyingi sana za hesabu ndo zinaamua bila kufikiri. Let us vote here

 
Kwani Yanga inahitaji Washambuliaji wangapi? Dube au Baleke?

Dube ni mzuri kuliko Baleke na Baleke ni mzuri kuliko Musonda. Ni vyema zaidi kama tukamsajili Dube na tufaye swap ya Kinzumbi kwa Musonda.
Musonda ni mzuri kuliko Baleke.
Musonda anakupa vitu vingi mkuu kuliko Baleke.
 
Back
Top Bottom