Swala la nyongeza ya mshahara wafanyakazi hawataki ufafanuzi. Haina tija na haitoshi

Huenda meimosi ikaongezwa tena. Hiyo elfu 20 inayolaaniwa haikuwepo for 5yrs na kazi mlifanya hamkuacha.
Mfumuko wa bei haukiwa katika Hali hii. Ujue. Najaribu kuvaa viatu vya watumishi naona vinavyobana!!!
 
Reactions: Tsh
Na huyo ndio tatizo kubwa,alipaswa aondoke madarakani kwa kumfanya Rais aonekane ni Muongo,amemfanya asiaminike tena,kila hotuba zake watakuwa wanamchora tu kama ilivyo kwa mzee wa Luangwa kule Lindi
Kaweka kodi kila sehemu sizizoendana na kipato cha watu wao makato ktk benki tatizo binafsi nilitaka kununua salio Nmb mobile nikatakiwa nilipie 100 kila nikiingia nikaweka 500 mwisho najibiwa huduma haijawezeshwa 500 imeenda na 7000 ipo kwenye acc.
kifupi mama kama ana washauri angemweka mwenye uwezo wa kufikiri pale wizarani binafsi mkenda naona anajielewa ila taaluma yake sijaijua.
 
Rais anayewadanganya watu wake wasomi.....,J.K tubadili katiba ugombea tena...,maana wote waliofata baada yako ni vituko....
 
Uko kwa ajira mpya wanalia no hela ya kujikimu no salary masikini wataishije ugenini huko hususanj walioenda mbali na mwakwao
Ajira mpya kawaida kukosa mshahara wa kwanza ila pesa ya kujikimu ni miyeyusho ya halmashauri
 
Mfumuko wa bei haukiwa katika Hali hii. Ujue. Najaribu kuvaa viatu vya watumishi naona vinavyobana!!!
Hii si sababu, Mfumuko wa bei wakati wa JK ulikuwa chini kuliko sasa, JK aliongeza mishahara na walimtukana na kutishia kugoma ila kazi hawakuacha.
 
Hii si sababu, Mfumuko wa bei wakati wa JK ulikuwa chini kuliko sasa, JK aliongeza mishahara na walimtukana na kutishia kugoma ila kazi hawakuacha.
Kwa hiyo unawashauri wafanyeje sasa hivi maana hii si awamu ya Kikwete!
 
Reactions: Tsh
Aliyetangulia alisema wazi "sitoongeza" tofauti na "nitaongeza 23" halafu anaongeza 5, angesema nitaongeza elfu 10 kwa kila mtu nani angelaumu? Anaona watumishi wooote wajinga fulani hivi, Uongo uongo kwa mwanamke ni sifa mbaya sana!
 
Hakika aisee,naanza kupata shaka nae sana huyu kiongozi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…