Swala la Watanzania kuto kuunganisha Mitaji yao ni sawa na Kujichimbia Kaburi la Biashara


Ndo kisingizio, Mimi napingana na wewe kwa 100% na hii ndo inatumika kama ngao ya kuhararisha watu kutengana.

Mkuu hivi watu kama 5 wameunganisha Mitaji yao pamoja na kuunda kampuni na wamegawana hisa kulingana na mitaji na katika kampuni ameajiriwa Mkurugenzi mtendaji, Kuna secreatary, ana wafanya kazi wengine, na katika kampuni umewekwa wazi kabisa kwamba mgao wa faida utakuwa kama ulivuo ainishwa kwenye katiba, sasa kurushana kuna toka wapi?

Huu ni uoga wa hali ya juu, hamuwezi unagana mkaanzisha kampuni then Murushane, huko kurushana kuna kuja vipi wakati kampuni inaendeshwa kwa mujibu wa Katiba?

Mfano

kampuni inashare 10,000

Wamiliki

1. Anashare 3000
2. Anashare 2000
3. Anashare 2500
4. Anashare 1000
5, Anashare 1500

Na watu wanagawana Faida kwa % ya share walizo nazo baada ya kuwa wametenga fedha kwa ajili ya kuendeleza kampuni, make kampuni hawagawani faida yote kwa asilimia 100 wanaweza kugawana asilimia 60 ya faida na nyingine ikawa ni kwa ajili ya kuendeleza kampuni, Sasa naomba unijibu kurushana kuna anzia wapi na kunaishia wapi
 
hapo nakubaliana na wewe kwa mfumo wa LLC, hapo tunaweza jitahidi lakini ujue watu wengi niseme asilimia kubwa wanafanya biashara ya (Sole Ownership), sidhani kama hilo ni neno sahihi...au wengine kwenye hizi biashara za kifamilia na wengi hawa opt kwneye hizo corporations..na wengine hazija acquire legal entity..yan daah
 
Watanzania tumezoa Partinaship za mfukoni, watu wanaounganisha mitaji bila kuwekena katiba ya kuwaongoza kwa nini msirushane? hata wazungu hawawezi ungana bila kuwekeana mikataba na kusaini MOU
 

Huo mfumo wa Sole ndo huo unao tumaliza kwa sababu stilii unakuta mitaji ni midogo, Kwa Nchi zingine Familia nyingi sana zina Kmapuni tena ndo rahisi kuliko zote, lakini Tanzani cha kushangaza unaweza kuta watu wafamilia moja wana compete katika soko yaani wao kwa wao ni competitors kitu ambacho hakipo mahali pengine, Chukulia mfano wa Mabasi,

Kuna kampuni kama nne au tano ni za watu wa familia moja na waote wana mabasi ya Arusha -Dar hii ni ajabu sana kwa nchi zingine lakini huku Bongo ni kitu cha kawaida kabisa kukuta Baba anamiliki Hotei mtaani na Mtoto anamiliki hoteli hapo hapo mtaani
 
Chasha, umesema maneno mazuri,
naomba Mamndenyi niunganishe mtaji na Chasha ili tufanye kazi,
kama kweli uliyoyaandika umemaanisha mimi nipo sawa japo sina hela mkononi but
nina mzunguko wa hela.

 
Last edited by a moderator:
Ttz kubwa watz ni kama vile wtt wa mama na baba 1.tumeumbwa na maneno mengi sn lkn waoga mno wa kuthubutu.hapa tunaoneshana uwezo wa kufikiri tulionao tu.ndio maana hakuna mpk sasa ktk hoja hi aliyetoa angalau mwanga/njia.me nashauri watu wenye nia ya dhati na wachapa kazi.tupange watu wengi wa kutosha tuandae warsha au kikao tuungane hata 100.then tupeane task .simply tunaweza kutengeneza mtaji wa kulima eka 40 za mpunga na 60 za mahindi n.k.kwa kuanzia.anza kuunga mkono hoja
 

Mkuu wewe labda ni Mgeni humu, Hili lisha pigiwa kelele mpaka basi, mimi mfano nilileta thread humu ya Kuhusu watu wakutane kikanda au kimkoa means

1- Arusha wanaungana na Manyara, Tanga na Kilimanjaro

2. Dar na Moro pamoja na pwani

3. Mwanza na wenzake

4. Mbeya na wenzake

Mkuu walio respond kwa kuchangia tu hawakufika kumi na walio kuwa tiyali kwa Arusha ni Mmoja tu, sas hebu cheki hapo, so some time inabidi mtu upambane kivyako ingawa ni ngumu na kwa mbeleni ndo kuna Ushindani mkubwa na wa hatari sana,

Watanzania tuko Bise na Mambo ya Ajabu kweli, mimi kuna watu tulipanga kuonana nao huku Arusha, Lakini cha kusikitisha na kukatisha tamaa mtu anakuambia anenda kwenye Ubarikio, mara kipa imara, mara Harusi mara sijui nini, ni ishu za Ajabu kweli, na si dhani kama Kuna nchi inaendekeza Sherehe kama Tanzania, kwa Africa Mashariki Tanzania tunaongoza kwa Kuendekeza sherehe zisizo kuwa na Maana kabisa, wewe imagine mtu anakopa benki au anauza Kiwanja ili amfanyie ,mtoto wake Ubarikio, ni ishu za ajabu kweli,

Kwa kifupi Watanzania Tunaendekeza sana Sherehe, wewe imegine mtu anafunga safari kutoka Arusha hadi Dar kwenda kuhudhuria Kipaimara tu, kwenda kula Pilau na kateketeza pesa za kutosha, mimi nimekaa Kenya kwa muda hakuna huu ujinga wa Tanzania na kote kuna haya haya makanisa ya Roman na Lutheran, ila cha kushangaza huku Tanzania ndo haya makanisa yanaendekeza sherehe za ajabu sana

Ila huyo mtu mwambie Atoke Arusha hadi Dar kuzungumzia ishu za Ujasirimali, hatakuelewa kabisa na atatoa visingizio vya kufa mtu, kwa kifupi ndo hivyo

So mkuu huwezi waita watu wakaja hata siku moja, Ila waambie kuna sherehe mtu atasafiri kutoka Mtwara hadi Arusha kuja kula tu na kurudi, na Nchi kama Kenya hapa ndo wanapo tupigia bao, wakati Tanzania watu wako bise na sherehe wenzetu wanafanya Production,

Mkuu so inasikitisha sana na inahuzunisha sana, ILA the time is coming, ambapo tutakuja kukumbuka sana hizi thread na michango ya watu humu, sio leo wala kesho ila kuna siku

 
Chasha, umesema maneno mazuri,
naomba Mamndenyi niunganishe mtaji na Chasha ili tufanye kazi,
kama kweli uliyoyaandika umemaanisha mimi nipo sawa japo sina hela mkononi but
nina mzunguko wa hela.

Mkuu wewe sijakusoma, huna pesa lakini unamzunguko wa pesa? ok ni wazo zuri sana mkuu, ila mimi niko Arusha, na ishu ya kuunganisha mitaji ni nzuri kwa watu walioko eneo Moja, mfano watu wa Dar wanaunganisha, Waru wa Mwanza wanafanya hivyo, Aruhsa wanafanya hivyo ,Mbeya na kazalika,

Kutoka hapo sasa ndo inaweza fuikia kuunganisha makampuni hata kutoka mbali, tatizo ndo kama hivyo mkuu hakuna anaye elewa somo, cha msingi tusubiri tu hao wawekezaji wanao kuja pamoja na wachina watukimbize mchaka chaka ili tuamke
 
Nimelipenda sana hili wazo..nachonga na rafiki yangu mmoja tuweke nguvu na kufanya biashara fulani. Ari na motisha tunayo sana.
 
Chasha ok lakini sijui kama wabongo wanathubutu,
akitokea tutafanya.

 
Last edited by a moderator:

Mkuu,
Kila mmoja aanzie alipo, angalia hiyo red part. Nawazimia sana wanaoanzia chini na kukua kwa hatua hadi wanafikia viwango.Kuungana kuna baki kuwa kwa mhimu sana kwa ulimwengu wa sasa.
 

Kuna watu wanakubali kukutana,wanapanga mipango safi hadi raha. Shida inakuja ktk utekelezaji wa maazimio, utasikia mkuu tuko pamoja usikonde, siku zinakatika, mwezi na hatimaye wale wachache hukata tamaa. Kwa uzoefu kidogo nilio nao ni kwamba ktk kuunganisha nguvu,kuna kuwa na asilimia ndogo ya wanaomaanisha, wengi huwa wapo kuvizia matokeo, matokeo chanya kidogo tu basi wapo ktk kugombea ukubwa, matokeo hasi hutawaona.

La pili ni hii tabia ya wengi kutaka kushiriki kila fursa inayojitokeza mbele yake. Akisikia kuna beach plot anataka, siku hiyo hiyo akisikia kuku wa malawi wanalipa naye yumo, kesho asubuhi akiambiwa Deci wanagawa hela yumo, matokeo hata ile plot ya beach inauzwa kwa sababu hana jeuri ya kuiendeleza. Sisemi watu wasiwekeze,nasema wekeza/fanya sawa na ubavu wako kikamilifu.
 
Tatizo laweza kuwa bad experience, lack of proper entrepreneurial education, entrepreneurial spirit, lack of role model....
 

Hata sisi tunakutana, kwa mfano humu jamvini kuna uzi wa chai day, siku hii hutokea mara moja kwa kila mwaka.Tunakutana,tunapanga,tunachambua changamoto.

Chai day itafanyika tena 2013, lakini pia tulikutana na tukaanzisha JE saccos, au sio sisi, tulikutana tukaanzisha shamba la jamii, hata kama asilimia ya washiriki ni ndogo, ni kwa sababu nyingi ambazo sio rahisi kuziondoa mara moja.

jambo lingine, watu wanataka mkutano/kikao kiitishwe na mtu mwenye jina kubwa ktk jamii, basi hapo watu kibao watakuja kwa matarajio ya kutumia jina la huyu aliyewaita. Tuitane sisi wenyewe akina yakhe. Hawa wakubwa wana mambo mengi sana wanatuchelewesha.
 

Mkuu ni kweli kabisa, watu wanataka wasikia Mzungumzaji atakuwa Mr Mengi hapo utawaona watu, na mikutano kama hii ndo ingekuwa njia pekee ya kusaidiana na kutatua baadhi ya matatizo, hakuna njia nyingine, Ila kwa mimi pamoja kwamba ni Dar ila ya mwakani mungu akipenda nitahudhuria hiyo tea day
 

Karibu sana mkuu, plan ni kuifanya february 2013
 
mimi nilishaungana na wenzangu miezi michache iliyopita na sasa naona mipango yangu ya miaka 7 ijayo inafanyika ndani ya miezi, msilalamike tatizo la kukosa mtaji/mkopo.. asasi nyingi sana za ndani na nje zinatoa fedha kwa vikundi na si kwa mtu mmoja. Pia kuna misamaha ya kodi inatolewa kwa vikundi vya wajasiriamali... serikali yetu ni sikivu lakini sisi si wasikivu
 

Nitakuwa sijakosea nikisema ww mwenyewe Narubongo umekuwa wa kwanza kuweka ahadi ya kuwa mwaminifu kwa kikundi chako. Mungu hawezi kukupa partiner mwaminifu kama ww mwenyewe sio mwaminifu. Mkuu songa mbele bila kuogopa na uwahimize wenzako na kuwaonyesha kuwa mtafanikiwa kwa kushikamana.
 

Mkuu hongera sana kwa hilo kikubwa kama malila alivyo sema wewe unatakiwa kuwa kiongozi wa mfano katika mabo yote
 


Mkuu hongera sana kwa hilo kikubwa kama malila alivyo sema wewe unatakiwa kuwa kiongozi wa mfano katika mabo yote

wakuu huu ni wakati wa vitendo, nilishawahi kujaribu kuunganisha mtaji na wenzangu lakini kosa nililolifanya lilikuwa ni kuomba ushauri kwa watu wangu wa karibu..cha muhimu ni kuchagua mtu mwenye historia nzuri, aliye serious na kazi na mwenye njaa kali ya maendeleo hata kama hana fedha nyingi ya kuwekeza mchukueni tu c'se yeye ni mtaji tosha, mkiona mtu yupo busy sana na shughuli zake nyingine huyo hafai kuungana nae, ... mnatakiwa kufanya vikao vya mara kwa mara mkiwa wote pamoja ili kuepuka maamuzi ya mtu mmoja kwenye shughuli za kikundi

kwa wale wenye interest na kilimo/ufugaji/maliasili etc mliopo mikoani/wilayani kwenu mnaweza kutembelea ofisi za kilimo, maliasili, ufugaji kama kikundi huko kuna fursa nyingi sana na mtasaidiwa tuache kulalama ardhi inauzwa kwa wageni wakati wewe hujui hata ofisi ya kilimo ipo mtaa gani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…