mcshonde
Member
- Jul 15, 2022
- 66
- 154
Mwanangu alifika eneo husika akiwa amenyuka uzi alioazima kwa jamaa aitwaye Omari. Huyo Omari alikuja chuo kutalii, yani target yake ni GPA ya chini kabisa inayoruhusu mwanachuo ahitimu. Tuachane naye huyo mtoto wa kishua, turudi kwa mwanetu ambaye alikuwa anajifuta kijasho chembamba huku mkononi akiwa na nakala tatu za CV yake ya kurasa 5; nusu ya ukurasa wa kwanza pekee ndio ulikuwa na taarifa zake binafsi pamoja na uwezo wake, lakini zilizobakia zote zilikuwa na “projects” ambazo angezifanya endapo angepewa nafasi na benki hiyo. Alipewa nafasi ya kujielezea kidogo na ikafika muda wa kupigwa swali; swali ambalo kwa mbali unaona halihusiani na mambo ya benki.
Aliulizwa
“Hebu fikiria unatoka Iringa kuja Dar kwenye kikao cha dharura, na unafika mikumi tairi ya mbele ya gari yako inachomoka na nati zote zinapotea kabisa. Sasa kama hakuna msaada wowote utakaopata hapo mbugani, ni wewe tu, tairi na spana yako, utafanyaje utoke hapo uwahi kikao?”
Mwanetu kichwa kilifanya kazi fasta kama kompyuta yenye RAM kubwa na Processor ya maana. Alijibu na hapo hapo wakamwambia umepata kazi. Mwanetu alimalizia mwaka wa tatu akiwa analipwa mshahara. Huwezi amini jibu alilipata kutoka kwenye stori za washkaji walipokuwa wanakula “mdudu” kwenye bar moja inaitwa Waswanu. Kila mtu na riziki zake ila ongea na watu vizuri; kila experience unayokutana nayo inaweza kukusevu baadae.
Unafikiri mwanetu alitoa jibu gani?