Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Na. M. M. Mwanakijiji
Nakumbuka zamani kulikuwa na watu wachonganishi - najua bado wapo. Watu hawa kwa asili yao wanapenda ugomvi na wakati mwingine wanachochea ugomvi unoge ili wao wafaidike kwa namna fulani. Wanaweza kumfuata na kumuambia mtu:
"Aisee unajua jamaa anasema we ni wa hovyo kabisa" wanaondoka na kumuacha jamaa anashangaa. Wanamuendea yule jamaa mwingine.
"Aisee jamaa ansema ati unamuita yeye wa hovyo, ni kweli". Ndipo mambo yanapoanza mwisho wa siku jamaa wanamuambia. "Aisee amesema akikuona atakukunja!!". Jamaa anaanza kupata munkari. Anatuma ujumbe na kuwaambia wamwambie "mahali popote na saa yoyote yeye hatishwi".
Nakumbuka jamaa ilianza hivi hivi mwisho wakaweka miadi baada ya shule, wanafunzi wote walijua kuna ngumi ztapigwa. Pembeni ya jumba moja gofu na hakun watu wazima watu wakaweka mduara na mchonganishi nambari moja akachukua mchanga akaweka kiganjani na kuwataka jamaa wazipige; lakini kama kweli lazima "wapete". Huyu akapeta, na yule akapata.
Mwenye maneno mengi akaanza kutanua misuri, mara akavua shati, akaanza kujifanya yeye Bruce Lee!! Mara anazunguka mashabiki wake wakishangilia. Yule mwingine naye akaanza kukunja tu shati lake anamuangalia jamaa anavyokwenda kwenda kwenye kilingo. Jamaa akaja mzima mzima kumvaa akamkwepa utadhani Steven Seagal! Na kwa madoido kama ya Jean Claude Van Damme akamtwanga ngumi moja jamaa alitoka mkukuu hadi akahama shule... heshima ikawekwa. Na wambeya wakanyamazishwa.
Hawa jamaa inabidi wazipige tu wenyewe ili hatimaye waheshimiane na dunia itulie. Mikwara mingi inaturusha roho bure tu. Kama wote wanadai Mungu yuko upande wao basi ama ni Mungu kigeugeu au mmoja hana Mungu au wote hawana Mungu!