Swali fikirishi juu ya mabingwa

mnadhimu mkuu wa jf

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2017
Posts
759
Reaction score
285
Habari zenu wapenda soka wote popote pale mlipo na wapenda michezo mingine pia wasalaam, wakuu kumekuwa na swali fikirishi ambalo linanisumbua ubongo hivi mwaka huu endapo simba atatwaa ubingwa wa ligi kuu na yanga akakamata nafasi ya 2 ina maana wote watakuwa na vigezo vya kwenda club bingwa africa?

Sasa na endapo kwenye fainali ya kombe la fA bingwa akawa yanga na simba akakamata nafasi ya 2 pia wote wanastahili kwenda shirikisho Afrika ss je mgawanyo wa timu hapo utafanyikaje ili kupata timu 2 za mabingwa africa na timu 2 za shirikisho africa naomba mwenye uelewa zaidi juu la hili atoe ufafanuzi.
 
Mkuu tatizo ninalo liona ni je yanga akiwa bingwa wa FA atakubali kwenda shirikisho halafu club bingwa apewe aliyeshika nafasi ya 3 kwenye ligi kuu.....
 
Hakuna swali fikirishi hapo ndugu.Iko hivi mabingwa inawakilishwa na alieshika nafasi ya 1 na 2 kwenye ligi na shirikisho inawakilishwa na bingwa wa FA na alieshika nafasi ya 3. Endapo bingwa wa FA ni yule alieshika nafasi ya 1 au 2 basi shirikisho itawakilishwa na alieshika nafasi ya 3 na 4. Hakuna option kwamba eti klabu inachagua kwa kushiriki kati ya shirikisho au klabu bingwa.
Nyinyi(yanga) fanyeni ulozi tu(joking) huko kigoma ili mchukue FA lakini klabu bingwa lazima muende mkapambane na akina Wydad.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…