Swali fikirishi: Kitendo cha Kangi Lugola kumfananisha Magufuli na Yesu, sio kwamba ni maono ya mwisho mchungu wa utawala wa Magufuli?

Swali fikirishi: Kitendo cha Kangi Lugola kumfananisha Magufuli na Yesu, sio kwamba ni maono ya mwisho mchungu wa utawala wa Magufuli?

Watoke hadharani wakanushe...
Kwan ni tuhuma? Hapo wewe unajiongeza mwenyewe! So siku nyingine wakimwita jina lingine akanushe tena! Atajitokeza hadharani kukanusha mangapi? Wewe ni mtu mzima
Magufuli SIO Bwana YESU!
Ukipenda ulishike hilo ukipenda fuata kinyume chake!
Haya siku njema
 
Hii tafakuri imekaa kiimani zaidi, baada ya kangi Lugola kumfananisha Magufuli na Yesu Kristo. Nimejikuta najiuliza haya maswali na kwa kuangalia mazingira mapana ambayo taifa linapitia kwa sasa, inawezekana kabisa maneno ya Kangi Lugola yamebeba maono ya mwisho mbaya wa utawala wa Magufuli.

Sote tunamlaumu Kangi kwa kuongea kitu cha kijinga, lakini ki ulimwengu wa Roho, kila neno litamkwalo linabeba maono yanayokusudiwa.

Sote tunajua na tumesoma katika vitabu vitakatifu, safari ya Yesu hapa duniani. Namna maisha ya Yesu yalivokatizwa kwa mateso makali.

Lakini pia, miongoni mwa wanafunzi wa Yesu kulikuwepo na msaliti (YUDA) ambaye katika umbo la nje ndiye aliyefanikishwa kukamatwa kwa Yesu na kupelekea mateso yale.

Nadhani Kangi aliongea kwa utani, ila kunaweza kuwa kuna ukweli kwamba Magufuli amezungukwa na watu mithili ya YUDA ambao kwa namna moja ama nyingine ndio wafanikishi wa mwisho mchungu wa utawala wake. Sote tumeona, YUDA alivokuwa mtumishi mwema kwa Yesu hapo mwanzo, lakini wema wake ule ule ulijeuka baadae na kuwa usaliti mkubwa kwenye historia ya vitabu vya dini.

Kama ni kitu kingepaswa kumpa Magufuli mawazo ya kufikiri, basi nadhani hili swala la yeye kufananishwa na Yesu itabidi liwe la kwanza kwa yeye kulifikiria kiroho zaidi.

Ukichunguza vizuri kwa makini, watu mithili ya Spika Job Ndugai ambao wanasahau mpaka majukumu yao na kuanza kupiga tarumbeta hadharani kutaka Rais aongezewe muda wa kutawala, inakupa taswira halisi ya wenye mioyo ya kina YUDA ndani ya utawala wa Magufuli

Kwa tafsiri nyingine watu mithili ya Job Ndugai, Kangi Logala,... na wengine mithili yao, ndio wanajeuka YUDA taratibu mda unavozidi kwenda.
Takataka hii
 
Back
Top Bottom