Swali fikirishi: Komredi Polepole na Mama Lulida nao wataapishwa 'pale' walikoapishwa akina Halima Mdee?

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,307
Reaction score
25,932
Wawili hao: Pole pole na Lulida leo wameteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa mujibu wa nyaraka iliyotoa uteuzi wao, Wabunge hao wateule wataapishwa kwa mujibu wa Katiba, Sheria na Taratibu za Bunge.

Je, nao wataapishwa na Spika Job Ndugai palepale walipoapishwa akina Halima Mdee ambao baadaye walifukuzwa uanachama wa CHADEMA?
 
Upatikanaji wa kina Mdee na wenzake ulikuwa batili, waliandaliwa na kupatikana kihuni, ndio maana wakaapishwa gereji haraka haraka kuharakisha mambo, huyo Polepole na mwenzake wataapishwa ndani ya bunge na glasi za kunywea maji watawekewa.
 
Kwnza kija mdee waliapidhwa wapi

Ina maaana haikuwa bungeni?
 
Why not. Anything is possible under this regime.
 


Kwa vile hawa wateuliwa hawajaenda Bungeni kupitia dirishani basi automatically wataapishwa kufuatana na kanuni za binge
 
Upatikanaji wa kina Mdee na wenzake ulikuwa batili, waliandaliwa na kupatikana kihuni, ndio maana wakaapishwa gereji haraka haraka kuharakisha mambo, huyo Polepole na mwenzake wataapishwa ndani ya bunge na glasi za kunywea maji watawekewa.
I see
 
Yaani palepale pasipo na SIWA?
 
Mwambie Jiwe anamsahau sana Pascal Mayala , amegeuka njaa kwelikweli humu mtandaoni , asipomteua anaweza kuchizika , maana amekuwa Mayala kweli yaani njaa .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…