Heshima sana wanajamvi,
Leo Rais wa JMT kafanya uteuzi wa wabunge wawili.Mh Polepole na Mh Riziki Said kuwa wabunge wa bunge la JMT.
Kwanza napenda kuchukua nafasi hii kuwapongeza,bila shaka waheshimiwa hawa wabunge wateuli wanaweza pia kuteuliwa katika nafasi za uwaziri kamili au uNaibu Waziri.
Shaka haipo katika uteuzi lahasha,uteuzi wao upo na umezingatia katiba yetu tukufu ambayo Mh Rais wa JMT anazo nafasi kumi za kuteua wabunge.Natamani katiba mpya ambayo ingeondoa hizi nafasi lakini sasa hakuna mjadala kabisa.
Najiuliza Mh Spika Dr John Ndugai atawaapisha waheshimiwa wabunge wateule GARAGE kama alivyowaapisha Wabunge 19 wa viti maalumu.Natumaini Mh Polepole na Mh Riziki watakula kiapo ndani ya bunge la JMT kwa heshima zote za kibunge.
Naomba kuwasilisha kwa unyenyekevu wa kiwango cha SGR.
Ngongo safarini Dodoma kupitia Dar ofisi za Lumumba.