Swali fikirishi: Nikwanini CCM hawakuunga mkono maandamano ya kupinga utekaji na mauaji ya raia?

Tuambie ccm mnaandamana lini kupinga utekajaji?
 
One mistake One goal !
 
Hilo nalo neno 🙄 !
 
Mbona wewe ulishiriki kinaa na ukakamatwa.
 
Mbona wewe ulishiriki kinaa na ukakamatwa.
unaitisha maandamno kwa kuchochewa na kilevi wanachama wako wote wanakusaliti hakuna hata moja anaejitokeza kuandamana, halafu unabaki mwenyewe na unakamatwa polisi pekeyao 🤣

hili ni gundu au mkosi gentleman?
 
Swali fikirishi kama chama dola, (CCM), kinashindwa kudhibiti watu wasiojulikana, je vyama vya upinzani vinaweza kudhibiti wasiojukikana?,
Yaani kikosi cha utekaji kinaweza kulisimamisha bus na kujitambukisha wao ni akina nani na wanakusudia kufanya nini na wakatekeleza hivyo

Kesho yake aliyetwaliwa anatupwa akiwa amekufa baada ya kipigo na kumwagiwa tindikali na maisha yakaenda kama kwaida, (business as usual as if nothing happened)
 
Kagoshima heshima yako, swali ni zuri lakini nataka tufikirie pia kwenye maandamano watu wa mbele kabisa nadhani wangekuwa familia ya watu waliyotekwa kwani wao ndiyo wenye uchungu zaidi kuliko mtu yoyote mwingine kwa kupotelewa na wapendwa wao. Swala likiingia katika upinzani wa kisiasa basi linapoteza nguvu kwa wananchi wote kuliunga mkono, lakini kama familia za waliyotekwa wangeandamana nadhani hapo kila mtu angeliunga mkono.
 
Chadema wali miss calculate sana hii issues. Maandamano haya ili yalete tija ilitakiwa yaanzie msibani, Baada ya kuzika tu mnaondoka na ile mob yoteee kwenda barabarani, Wengine waunge kutokea hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…