Swali fikirishi: Upi ni urafiki wa ukweli kati ya AA, BB au AB?

Deejay nasmile

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2011
Posts
5,794
Reaction score
5,352
Katika maisha kuna kitu kinaitwa urafiki wa ukweli.yaani

Utakuta watu wameshibana hatari...alipo huyu na mwenzake yupo. Au mmoja akiwa na shida hata usiku wa manane mwenzake atapambana kumsaidia haraka(kutokupuuza mambo)

Kumbuka hapa naongelea URAFIKI SIO MAPENZI...

Sasa kuna jinsia mbili
KIUME: (A)
KIKE🙁B)

SWALI; ni urafiki gani ni wa ukweli,wa shida na raha,wa kudumu,wa uhakika,usio na majungu,masengenyo. Kati ya Jinsia Ya;
AA -(KIUME KWA KIUME)
BB -(KIKE KWA KIKE)
AB- (KIUME KWA KIKE)

URAFIKI GANI kwako ni mzuri zaidi...unafaa
Nasisitiza ni urafiki sio mahusiano ya mapenzi..

Haya mabest na mashosti karibuni
 
Mkuu hili swali lako halina majibu ya moja kwa moja yaani hapo hutegemea ni aina gani ya watu mmekutana bila kujali jinsia zenu ili mradi mmeendana ktk mienendo yenu basi urafiki wa kweli huja tu.

Ila kwa upande wangu sisi wa kiume AA kama tunakuwa na tabia moja na maelewano basi huwa tunakuwa marafiki wazuri sana yaani damu damu (AA)

Huu urafiki wa (AB) nauhakika amwezi kudumu muda mrefu sana bila kuzama kwenye mahusiano au hata ile sex partners.

Na huu urafiki wa (BB) hawa watu aisee hawachelewi kuingiziana fitna hasa mmoja wapo akifanikiwa, hapa tutaelewana vizuri kama umesikiliza ule wimbo wa nyota ndogo - kuna watu na viatu.
 
Kwa upande wangu Mimi kike na kike kutokana na hali ya urafiki wetu..na huyu kidawa wangu.
 
marafiki mnachaguana mkiwa mna resemble tabia pamoja, huwezi kua na urafikina mtu tena urafiki wa shida na raha awe tofauti na tabia yako hivo bas yategemea wewe ukoje kama msengenyaji na wewe utakua hivohivo

hivo kwangu kwa rafiki niliyenaye ni BB
 
Ni lini urafiki kati ya AB ukawa wa kweli bila kuwepo "Mapenzi"??!--- labda woote wawili wawe "sexually impotents", otherwise haakuna urafiki wa kweli kati ya AB.

Urafiki wa kweli unaweza kupatikana kati ya AA, na hivyo hivyo kati ya BB.
 
Nakumbuka sana nigaa wangu G,sikuwai kuwa na rafiki wa kweli Kama huyuu,nilipigwa kisu kwa ajili yakee.....na alikua dogo kwangu Ila man of action,nilipo yupo.rest in peace bro!ila Hawa marafiki wa ukubwani Ni wapombee na starehe tu,ukiwa huna huwaoni
 
Ni lini urafiki kati ya AB ukawa wa kweli bila kuwepo "Mapenzi"??!--- labda woote wawili wawe "sexually impotents", otherwise haakuna urafiki wa kweli kati ya AB.

Urafiki wa kweli unaweza kupatikana kati ya AA, na hivyo hivyo kati ya BB.
Sio kweli mkuu...mfano mm nikikuwa na rafiki yangu mmoja wa kike kwa muda mrefu sana hatukuwahi kujihusisha na mapenzi hata siku moja....zaiid zaid ndo kwanza nilikuwa namtumia kunitongozea wasichana wenzake...urafiki ulikuwa kupungua baada ya yy kuolewa na mume wake kumpiga biti akidhan kuwa na mm napita nae
 
Ilikuaje tena visu hvo
 
Kwa upande wangu mie urafiki wa kweli upo AB.
 
Kwa upande wangu mie urafiki wa kweli upo AB.

I think AB can be comfortable for u but not the guy. It only happens after being friend zoned, ila initial intention was not to be just friends...
 



Kama ungejaribu kupima kwa kina kile nilichoandika kamwe usingekuja na huo mfano hai wako, kifupi huo mfano wako ni kama unaniunga mkono kile nilichoandika.

Haiwezekani aslan kwa mwanaume rijali akawa na urafiki na mwanamke mrembo bila kutamaniana kimapenzi, ninachokiona kati ya urafiki wenu wa zamani wewe na huyo demu ni kama urafiki wa wavulana wawili, yawezekana huyo demu hakuwa mrembo usoni kwako ndiyo maana akawa ni kuwadi wako, waswahili wanasema fimbo ya mbali haiui nyoka, sasa ilikuaje uchukue fimbo za mbali wakati fimbo ya karibu ulikuwa unayo???!!, au (ashakum) huyo demu alikuwa ni dada yako, au mama yako mdogo nk??!!!, kifupi ni kwamba usemacho hakiingii akilini.

Huyo demu hakuwa attractive to you, hiyo ni sawa kama vile ulikuwa upo pamoja na mwanaume mwenzako, kimsingi unakubaliana na mimi kwamba hakuna urafiki kati ya AB bila kuhusisha mapenzi yaani urafiki wa kweli kati ya AB hushadidishwa na mapenzi (love/ conjugal relationship).
 
Alikuwa mrembo sana..huwezi amini ila ndio hivyo sikuwa na hisia nae,wala yeye hakuwa na hisia nami za mapenzi..japo nilimpenda alinipenda hatari
a
 
Urafiki wa kweli wa AB wawe watu ambao wanatakana ila hawaambiani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…