MK254
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 32,408
- 50,809
Nimeisikiliza hotuba ya Profesa Kabudi wa kutokea Tanzania, kwa kweli ametiririka maneno yenye hekima na kutuasa Wakenya tuwe kimoja, pia akamsifia sana Rais wetu Uhuru kwa kukubali kujishusha na kuweka uzalendo mbele na kukaa meza moja na wapinzani kwa minajili ya vipaumbele vya taifa.
Nikawa najiuliza mengi, maana taarifa tunazozisoma kuhusu Tanzania zinakinzana na huu ushauri wa Professa kwa asilimia 100%, kule watu wamegawanyika kwa misingi ya vyama, yaani juzi tu chama kinachotawala kimeibuka na ushindi wa asilimia 99% baada ya upinzani kutunishiwa misuli hadi wakajiondoa.
Tumekuwa tukiona matamko na mikwara ya waliopo kwenye dola wakiweka wazi bila kuremba kwamba maeneo ya upinzani yanakosa maendeleo kama adhabu ya maamuzi yao mabaya.
Mifano ni mingi tu ambayo tunaisoma inayodhihrisha demokrasia ilivyofukiwa kwa Wabongo, sasa professa, hivi alikua anatuma ujumbe kwao nyumbani kinyemela au alikua na maana gani.
Pia juzi tuliona Spika wa Tanzania alitutembelea hapa Kenya na kusifia sana mfumo wetu wa kurusha shughuli za bunge mubashara, licha ya yeye kule kwao kubana hayo hayo aliyokuwa anasifia, sielewi mbona wakija huku wanasifia mambo ambayo wenyewe kwao wanayakandamiza na kuyadidimiza.