Chumchang Changchum
JF-Expert Member
- Nov 1, 2013
- 5,988
- 6,226
Nyinyi ufanyieni kazi huo ushauri haya ya kwetu tutayaweka sawa.. Ok
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kumbe unasikiliza ya MtandaoniNikawa najiuliza mengi, maana taarifa tunazozisoma kuhusu Tanzania
Kumbe unasikiliza ya Mtandaoni
Naamini umeshatembelea Tanzania,na umeiona tofauti yetu na yenu,ila tu hutaki kusema
Sitosahau nilitumwa kazi nairobi,mwenyeji mkikuyu,bosi jaluo,yule mkikuyu alinibabaisha sana mpaka tunafika ofisini hakuingia kabisa ofisini kwa jaluo.kwetu hakuna upumbavu huu
Asante sana na wewe kwa kuliona hili, huyu jamaa anafanya mambo ya hatari na ajabu sana, anajifanya kumuenzi na kumtaja sana Nyerere lakini anafanya kitu ambacho nyerere alikipinga kwa nguvu zote..Inasikitisha sanaalimwapisha jaji mmoja mchaga, akamsifia kwa kupigana na rushwa mpaka watu wakasema "huyu mchaga gani hataki rushwa?..."
jana pia nimemwona anahutubia Igunga kwa kilugha, nikawa najiuliza, Igunga huko anaongea lugha gani, ghafla mzee akaona hapati muitikio, akawauliza, Kisukuma si mnakisikia? Sasa kama huna hakika Igunga wanasikia Kisukuma, kwa nini usiongee Kiswahili?
Alikuwa akijitetea ucheleweshaji wa mradi wa maji ya Victoria, akawaliwaza kwa Kisukuma kwamba hata shamba la mpunga linaanza kwa kuandaa shamba kabla ya kupanda na kuvuna... akielezea failures za serikali yake anatumia karata ya ukabila kutafuta sympathy kuwakumbusha ni mtu ni wao, anawaona ni wakulima ma primitive ambao akiongea nao lugha za kienyeji ata connect...
Sijakataa Kenya kuna ukabila,Tatizo la ukabila la Kenya sio la kusadikika au kudhani, ni la muda mrefu toka nchi hio ipate uhuru wake.
Tatizo hilo la ukabila limekuwa lilisababisha maelfu ya raia wa Kenya kuwa displaced ndani ya taifa lao na pia watu wengi kupoteza maisha.
Tatizo hilo la ukabila limesababisha kabila moja la Kikuyu kutawala Kenya toks nchi ipate uhuru (ukimuondoa Moi).
Kenya si ndio ilikua na best constitution lakini ineshindokana kwa sababu ya huohuo ukabila, ndio maana wanakuja sasa na BBI ili kusawazisha mambo.... Johnny Sack,
Asante sana na wewe kwa kuliona hili, huyu jamaa anafanya mambo ya hatari na ajabu sana, anajifanya kumuenzi na kumtaja sana Nyerere lakini anafanya kitu ambacho nyerere alikipinga kwa nguvu zote..Inasikitisha sana
asante sana mkuu Tindikali, nafurahishwa sana kuona kuna Watanzania ambao wapo concerned kweli na mshikamano na umoja wa taifa letu kama wewe. Nakumbuka pia alipokuwa Dodoma alimlazimisha Ndugai kuzungumza kigogo, aipokuwa Nyanda za juu kusini akamlazimisha yule waziri Hasunga kuzungumza kikwao, pamoja na yule Kamwele. Sijui anafanya hivyo huku akijua athari zake ama anafanyaakiwa hajuiyes, nilimwona, its was so obvious
kuna yule Mama wa Kihehe yuko Kahama, Rais akamuuliza unatokea wapi halafu akamsemesha Kihehe, Mama akam blow off, akamwambia nimetoka huko Iringa zamani, sikikumbuki Kihehe...
dada mwingine Rais kamuuliza kabila akasema Muhaya, akamsemesha matani ya Kihaya, dada akam blow off, hakujibu Kihaya, dada alikuwa amenyosha kidole kumueleza Rais issue ya mme wake aliyeuliwa na gari la traffic police aliyekuwa kalewa, na bado ananyimwa haki, aliongea analia machozi, mtoto mgongoni analia machozi na mwingine kamkokota analia machozi, needless to say, hakuwa na mood wala muda wa matani ya Kihaya kutoka kwa Rais...
Muda huo huo Rais anawauliza watu Shinyanga kama ni Wasukuma na kuwasemesha Kisukuma Waziri Palamagamba Kabudi yuko Kenya anasema katumwa na Rais kuwaambia Tanzania hatuulizani kabila!
MK254,
BBI ya Kenya imeanza kuwa na mguso Tanzania, baada ya Mwenyekiti wa CCM katika hali ambayo haijaonekana kwa muda mrefu alionekana kufuata siasa za hand-shake na ni kiashirio pengine BBI imeanza kuingia Tanzania kama alivyosema Profesa Palamagamba Kabudi kuwa BBI ni ya Afrika Mashariki.
December 9, 2019
Mwanza, Tanzania
Magufuli alivyowaona vigogo wa CHADEMA alijongea na kuwasalimia
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli, amesalimiana na baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani katika sherehe za miaka 58 ya uhuru.
Vigogo wa chama cha CHADEMA waliopata nafasi ya kusalimiana na Rais Magufuli ni Mwenyekiti Kanda ya Kati CHADEMA Lazaro Nyarandu, mbunge John Heche, Meya Boniface Jacob, mbunge Joseph Mbilinyi Sugu, mbunge John Mnyika na mbunge Godbless Lema katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
Pia Mwenyekiti wa Taifa CHADEMA na Kiongozi wa Upinzani Bungeni (KUB) Mh. Freeman Mbowe (MB) aliitwa kusalimia halaiki wa watu uwanjani CCM Kirumba na watanzania kwa jumla waliokuwa wakifuatilia sherehe hizo za uhuru wa Tanganyika majumbani mwao ktk televisheni zao.
Katika sherehe hizo za miaka 58 ya uhuru wa Tanganyika kulikuwepo pia mabalozi wa nchi za Afrika, Ulaya, Marekani ya Kaskazini, Asia na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa kama Benki ya Dunia, Umoja wa Ulaya n.k
Source: Global online TV