Swali fukunyuzi: Kabudi katuasa vizuri sisi Wakenya, ila mbona huko kwao Tanzania hawazingatii haya haya anayoturai?

Nikawa najiuliza mengi, maana taarifa tunazozisoma kuhusu Tanzania
Kumbe unasikiliza ya Mtandaoni
Naamini umeshatembelea Tanzania,na umeiona tofauti yetu na yenu,ila tu hutaki kusema
Sitosahau nilitumwa kazi nairobi,mwenyeji mkikuyu,bosi jaluo,yule mkikuyu alinibabaisha sana mpaka tunafika ofisini hakuingia kabisa ofisini kwa jaluo.kwetu hakuna upumbavu huu
 

Hivi mtandaoni wanatudanganya wanaposema CCM imeshinda uchaguzi kwa asilimia 99.9% baada ya upinzani kujiondoa kutokana na dhuluma.

Hawa watu wa mtandaoni wanatudanganya mengi sana, itakua hata hizi habari hapa chini wametunga wao na kutengeneza videos

https://www.jamiiforums.com/data/attachment-files/2019/10/2183667_VID-20191015-WA0037.mp4
 
Asante sana na wewe kwa kuliona hili, huyu jamaa anafanya mambo ya hatari na ajabu sana, anajifanya kumuenzi na kumtaja sana Nyerere lakini anafanya kitu ambacho nyerere alikipinga kwa nguvu zote..Inasikitisha sana
 
Sijakataa Kenya kuna ukabila,
Nilichosema ni kuwa kuna vitendo vingi anavifanya Rais ambavyo ndio vinaamsha hisia za ukabila. Na nimemkosoa Kabudi kusema Tz hatutukuzi makabila wakati boss wake aliyemtuma analifanya karibia kila mara
 
Asante sana na wewe kwa kuliona hili, huyu jamaa anafanya mambo ya hatari na ajabu sana, anajifanya kumuenzi na kumtaja sana Nyerere lakini anafanya kitu ambacho nyerere alikipinga kwa nguvu zote..Inasikitisha sana


yes, nilimwona, its was so obvious

kuna yule Mama wa Kihehe yuko Kahama, Rais akamuuliza unatokea wapi halafu akamsemesha Kihehe, Mama akam blow off, akamwambia nimetoka huko Iringa zamani, sikikumbuki Kihehe...

dada mwingine Rais kamuuliza kabila akasema Muhaya, akamsemesha matani ya Kihaya, dada akam blow off, hakujibu Kihaya, dada alikuwa amenyosha kidole kumueleza Rais issue ya mme wake aliyeuliwa na gari la traffic police aliyekuwa kalewa, na bado ananyimwa haki, aliongea analia machozi, mtoto mgongoni analia machozi na mwingine kamkokota analia machozi, needless to say, hakuwa na mood wala muda wa matani ya Kihaya kutoka kwa Rais...

Muda huo huo Rais anawauliza watu Shinyanga kama ni Wasukuma na kuwasemesha Kisukuma Kabudi yuko Kenya anasema katumwa na Rais kuwaambia TZ hatuulizani kabila!
 
asante sana mkuu Tindikali, nafurahishwa sana kuona kuna Watanzania ambao wapo concerned kweli na mshikamano na umoja wa taifa letu kama wewe. Nakumbuka pia alipokuwa Dodoma alimlazimisha Ndugai kuzungumza kigogo, aipokuwa Nyanda za juu kusini akamlazimisha yule waziri Hasunga kuzungumza kikwao, pamoja na yule Kamwele. Sijui anafanya hivyo huku akijua athari zake ama anafanyaakiwa hajui
 
MK254,

BBI ya Kenya imeanza kuwa na mguso Tanzania, baada ya Mwenyekiti wa CCM katika hali ambayo haijaonekana kwa muda mrefu alionekana kufuata siasa za hand-shake na ni kiashirio pengine BBI imeanza kuingia Tanzania kama alivyosema Profesa Palamagamba Kabudi kuwa BBI ni ya Afrika Mashariki.

December 9, 2019
Mwanza, Tanzania

Magufuli alivyowaona vigogo wa CHADEMA alijongea na kuwasalimia

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Magufuli, amesalimiana na baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani katika sherehe za miaka 58 ya uhuru.

Vigogo wa chama cha CHADEMA waliopata nafasi ya kusalimiana na Rais Magufuli ni Mwenyekiti Kanda ya Kati CHADEMA Lazaro Nyarandu, mbunge John Heche, Meya Boniface Jacob, mbunge Joseph Mbilinyi Sugu, mbunge John Mnyika na mbunge Godbless Lema katika uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.

Pia Mwenyekiti wa Taifa CHADEMA na Kiongozi wa Upinzani Bungeni (KUB) Mh. Freeman Mbowe (MB) aliitwa kusalimia halaiki wa watu uwanjani CCM Kirumba na watanzania kwa jumla waliokuwa wakifuatilia sherehe hizo za uhuru wa Tanganyika majumbani mwao ktk televisheni zao.

Katika sherehe hizo za miaka 58 ya uhuru wa Tanganyika kulikuwepo pia mabalozi wa nchi za Afrika, Ulaya, Marekani ya Kaskazini, Asia na Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa kama Benki ya Dunia, Umoja wa Ulaya n.k

Source: Global online TV
 

Hongera sana, hiyo vizuri, wote ni Watanzania na ni wazalendo, hamna lisilowezakana, taratibu tu hivyo na watakua kimoja kwa ajili ya maslahi mapana ya jamhuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…