Swali Fyatu: Furaha Kwishnei?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
33,771
Reaction score
41,027
Watu walishangilia na kugongeana bia..
Wapo waliocheka kwa sababu sasa wanaaenda kupumua kidogo...
Wapo waliofurahia hela kurudi mitaani aka "mzunguko wa fedha kuongezeka"...
Wapo waliosema "sasa hatufokewi foreign tena" ..na kuwa "nchi ina tabasamu".

Furaha imerejea tena, kicheko kimerudi....

Mara paap!

Wanung'unikaji wameanza tena, wenye kununa wameanza kukereka...hakuna jema mama anaweza kufanya...mama..hafuati njia wanayotaka aifuate... na gwanda la jeshi likawatifua (ntaligusa hili baadaye inshallah).

Kama alivyouliza jamaa mmoja...furaha Imeenda wapi? Kicheko kimepotelea wapi...

#mwachenimama
#mamasalama
#salamasamia
#tanzaniayasamia
 
Kuimba ni kupokezana.
 
Aiseee.

Kweli huwezi kushindana na nyakati.

Sasa hivi unaandika vi-threads vyako havina tofauti na vya Mmawia na johnthebaptist
 

Mpka Siku Simba Watakapo Amua Kuwa Na Waandishi Wao Ndipo Historia Ya Muindaji Itakapo Badilika;
 
Sasa hivi haufahamiki hata unachopigania , yaani umekuwa chawa kamili
 
Wewe binafsi ulikuwa upande gani?? Na je Hangaya mara tu baada ya kukabidhiwa kijiti alisimama upande gani na hivi sasa kaegemea wapi??

Ahadi alizozimwaga Kwa Watz na kuwafanya wawe na tabasamu aliziahidi mbele za Muumba wetu. Kilichokuja kimefanya akengeuke anajua mwenyewe. "Mungu ni Fundi kuliko Yeye" . Tunaendelea na maombi yetu.
 
Kiwango chako cha kupambanua mambo kimeshuka sana. Umeingiliwa kwenye ubongo unaelekezwa nini cha kuleta humu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…