Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,771
- 41,027
Na. M. M. Mwanakijiji
Sijui lipi ni bora katika siasa au yote ni sawa tu? Yaani, unamheshimu mtu si kwa sababu anastahili heshima hiyo bali kwa vile unamuogopa. Unaogopa huyo mtu atakufanya nini. Unajitahidi kumfurahisha kwa sababu hutaki achukie au akushukie. Akinuna unaweweseka. Unajua humpendi lakini ufanye nini wakati yeye kashika mpini.
Au, unamuonesha mtu mapenzi kwa sababu hutaki akufanye lolote na yeye hakufanyi lolote kwa sababu anaamini unamuo. nesha mapenzi. Unamsifia na kumuonesha heshima kwa sababu atakuzawadia mapenzi yake. Unataka na wewe akuone unampenda. Akikasirika anaweza kukunyima vitu na hilo wazo linakutisha.
Kumbe ukiangalia utaona kuwa heshima ya woga na penzi la kinafiki ni pande mbili za sarafu moja. Vyote viwili msingi wake ni khofu. Lakini, Kuna watu wanaamini kimojawapo ni nafuu.
Yaani, mmoja anaweza kukupa sumu kwa sababu hakupendi ila mwingine anaweza kukupa sumu ukiamini anakupenda.
Go figure.
MMM