Swali Fyatu: Wanaosali kwa Gwajima wako Dini Gani?

Swali Fyatu: Wanaosali kwa Gwajima wako Dini Gani?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
33,771
Reaction score
41,027
Nimekuwa nikijiuliza mara kwa mara toka wakati wa Sakata la kijana yule kutoka Kolomije...na kabla yake like suala la ushenga...na yale "maufundi"...

Sasa katika Sakata lililochukua sura ya kifamilia na Kikolezo cha Imani vinaniacha na maswali. Hivi Askofu Gwajima anatekelezaje lile Agizo Kuu katika huduma yake, ni kwa kiasi gani anasimamia ile amri ya pili kubwa inayofanana "na ile ya kwanza"?

Je, anasimamia vipi maneno ya Mtume Paulo kuwa kama mtumishi wa Mungu anahubiri kitu kingine is ipo kuwa "Yesu Msulubiwa" na "uweza wa kufufuka kwake"(1 Kor. 1:23). Na ni kwa kiasi gani Gwajima anajitahidi kujua mambo mengine nje ya lile jambo la kumjua "Yesu Msulibiwa"(1 Kor 2:1,2).

Lakini labda swali kubwa ni kwa safari wa Gwajima (sijui kama ni sahihi kuwaita warming au la) ni kwa kiasi gani wanamfuata Gwajima au Kristo au ni kwa kiasi gani wanaamini kwa matendo ma mahubiri yake anawaongoza kumfuata Kristo.

Kisiasa Gwajima ana haki ya kucheza na kufanya siasa kama wanasiasa wengine. Hili si tatizo kabisa. Linapokuja suala la wokovu labda tuulize maswali haya machache. Nje ya hapo na mimi nasubiri kusikia uhalalishaji wa ya Gwajima katika Imani? Anaongozwa na Roho Mtakatifu, Roho Mtakavitu, au yule roho machachari...Roho Mtakabifu?

MMM
 
Watakuwa CCM. Hata mzee Kingunge (rip) aliwahi kudai hiyo ndiyo ilikuwa dini yake.
 
Waumini wengi wa madhehebu ya Kikristo wana “itikadi” za kidini. Hawafahamu kwa kina madhumuni ya Ukristo na Kristo mwenyewe. Itikadi inaleta upofu. Ndio maana unaweza kuona kinachoendelea kikiambatana na vigelegele.
 
Wako dini yako. Kwani ulikuwa hulijui hilo? Eti swali fyatu 🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Waumini wa Gwajima ni wale wanaopenda umbea na mipasho.
 
Sasa kule bungeni nani anayeweza kutetea watu wa Imani.
Kama viongozi wa Serikali wamechanjwa nani atakayetoa sauti kuwatetea watu wasiotaka kuchanjwa yeye yupo na siasa kwa wakati maalumu na wakati wenyewe ndo huu.

ondoa shaka,
Jaribu kufikiri Bungeni wapitishe sheria Chanjo kuwa ya lazima Mbunge gani wa CCM atakayekataa kama wabunge wenyewe ndo hawa vigeugeu wazee wa Ndio .
Gwajima yupo pale kwa wakati sahihi
 
Back
Top Bottom