Swali Gomvi: Korona 2.0 kwani Rais Magufuli ni mbia wa maisha yenu?


Hatujitaji lockdown. Tunahitaji kukiri kuwa tuna tatizo na kisha kuchukua hatua (hasa za kitabibu). Kunawa mikono, kuvaa barakoa kufanya social distacing na kujifukiza ni mambo yaliyo mikononi mwa mtu mmoja mmoja! Huwezi kusema hakuna corona halafu ukasisitiza hatua hizo.

Kabla ya kutubu, kukiri ni mkosaji ni jambo la kwanza!!
 
Wewe uko nchi gani?
Huu ni mlipuko mpya wa waka 2021, siyo ule wa mwaka 2020.

Usipowatangazia wananchi kuwa kuna tatizo limejitokeza tena na hivyo watu wajihadhari wengi wataenfelea kuamini kuwa tulishaishinda orona mwaka 2020 na hivyo hakuna tatizo tena kumbe lipo
 
Kwahiyo maneno mengi kumbe umeukana leo msimamo wa rolimodo wako .
 
Lockdown siyo suluhisho zuri kwa aina ya maisha ya wengi wetu kwenye jamii yetu.
Kuongelea hadharani uwepo wa ugonjwa, kukumbushana njia zinazo sadikika kupunguza kasi ya maambukizi ndiyo suluhisho zuri kwa muda uu, na ndiyo zilitusaidia wakati wa wimbi la kwanza la COVID-19.

Hakuna ushahidi mzuri wa kisayansi na unao onesha sala zilitusaidia
 
Huku hakukuwa na utafiti lakini alipanga foleni ili apate kikombe cha Babu, lakini chanjo ya MABEBERU iliyofanyiwa utafiti anaikana! WANAFIKI bana!

 
Umemaliza kila kitu Mkuu

Cc
Washauri wa Mkuu
 
Kusoma masomo ya sayansi sio kuwa mwanasayansi. Kusoma sana msaafu hakufanyi mtu kuwa mtakatifu. Huyu hajawahi kuwa na hatakuwa mwanasayansi. Kuwa mwanasayansi ni mpaka wanasayansi waseme ni mwanasayansi!
Alifoji vyeti. Wapi ilipo thesis yake ya PhD?
 
Corona ya 2020 na hii ya 2021 ni ileile, njia za kujikinga ni zile zile, social distancing, barakoa nk... Sasa watangaze nini cha ziada?? Nini kimeongezeka kwenye korona hii?

Sent from my Android using JamiiForums mobile app
 
Hapa nimekuelewa na sitakuandikia gazeti refu kukujibu.

Ni kwamba, anayewaongoza waTanzania yupo kwenye madaraka hayo kwa njia batili kwa sababu kalazimisha kuwepo kwenye uongozi na waTanzania hawana lolote wanaloweza kufanya kumwondoa hapo hata kama wanaona anafanya makosa na anatabia zake mbaya asizoweza kuzibadili.

Njia unayopendekeza ni kwa waTanzania wampuuze, wasimsikilize, wafanye wanayoona yanawafaa wao, kila mtu kwa njia zake mwenyewe, kwani hakuna kiongozi mwingine wa kuwaunganisha wafanye mambo wanayoona kuwa ni kwa manufaa yao na taifa lao.

Usilopendekeza hapa kwa maksudi ni kuwasihi waTanzania waungane kwa umoja wao kukataa makosa anayofanya, bali unaona ni bora waendelee kuvumilia makosa anayofanya kwa wao kujifanyia ya kwao kila mmoja kwa njia zake mwenyewe azijuazo. Hupendekezi kwa umoja wao waungane na watafute njia za pamoja za kuondoa tatizo.
 
Nyie mashabiki mtapoteza wengi maana kila jambo mnaingiza ushabiki.
 
😂😂😂 Facts za wenye chuki na kinyongo😂😂, anyway v8 hazichukuliw zinanunuliwa, mm mwenyew nimejinunulia binafs ya kutembelea, fanya Kaz chuki ipungue
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…