Dark City
JF-Expert Member
- Oct 18, 2008
- 16,253
- 11,626
Hapo kahaba anakuwa anajua marital status ya huyo anayemegana naye au anakuwa hajui?
Manake katika mjadala wa jana na by extension huu wale ni kwamba huyo mtu wa pili anakuwa analala na huyo mwanandoa huku "akijua" kuwa huyo mwanandoa yuko kwenye ndoa.
Sasa kahaba unayenunua mtaani naye anakuwa anajua marital status ya huyo mteja ama?
Kahaba yuko kazini na hana sababu ya kujua marital status ya mteja wake,.. haimhusu kabisa...
Nimetumia mfano huo kuonesha kuwa kahaba hawezi kubeba makosa ya mteja wake. Anabeba ya kwake tu (kama yapo).
Mwanamke aliye nje ya mahusiano akitembea na mume wa mtu, anaweza kufanya hivyo huku akijua au la. Kama hajui, basi anabebe mzigo wake mwenyewe kama mfano huo wa kahaba. Ila kama anajua, atabeba pia lawama kwamba pamoja na kuwa amekwenda kinyume na maadili kwa kufanya uasherati, ameenda bali zaidi kwa kutembea mume wa mtu. Kwa msingi huo, anakuwa amemkosea mke wa huyo mwanamume pia. Kwani atakuwa amefanya jambo ambalo hapenda kutendewa.
Ila kama nilivyosema huko nyuma, huyo mwanamke hana kiapo au nadhiri ya uaminifu kwa mtu yeyote (including mke wa huyo mwanamue). Kwa maana hiyo, ana makosa ila hajamsaliti mtu (she has not cheated anyone)!!
Babu DC!