Kweli Mwanakijiji,
Maana kweli haiji,
Swali likizidi lahoji,
Jibu pia lisihoji.
Ya kale kutupa njia,
Na hekima kutujia,
Swali linapotujia,
Na jibu lipate njia.
Mpanda ngazi hushuka,
Mkwezi hutelemka,
Mimi siyo mahoka,
Ukajifanya kucheka.
Mwanamke kuwepo,
Na mwanaume kawepo,
Kama vile usiku upo,
Na mchana pia upo.
Nami nakuunga mkono
Wala sitalala pono,
Kujenga lugha nono,
Ifaayo kwa maono.