Bongotunacheza
JF-Expert Member
- Dec 7, 2018
- 1,821
- 3,980
Kama Mungu anajua kila kitu tangu mwanzo mpaka mwisho (anajua nani ataenda mbinguni/peponi na nani ataenda motoni kabla hata hawajazaliwa), je, kweli binadamu ana uhuru kamili wa kuchagua? Kama Mungu alishajua nitatenda dhambi fulani kesho na siwezi kubadilisha kile Mungu anachokijua tayari, uhuru wangu wa kuchagua uko wapi? Na kama sina uhuru kamili, kwa nini niadhibiwe kwa kufuata mpango ambao tayari ulishajulikana?
2. Kama Mungu ni mweza yote na pia ni mwingi wa upendo na rehema isiyo na mipaka, kwa nini anaruhusu watoto wadogo wasio na hatia wazaliwe na magonjwa na kutesa au kufa kwa njaa au vita?
Kama anataka kuzuia uovu huu lakini hawezi, basi yeye si mweza yote.
Kama anaweza kuzuia lakini hataki, basi upendo na rehema zake ziko wawapi?
3.Ikiwa mtu alizaliwa katika kisiwa kilichojitenga sana miaka 1,000 iliyopita, na akafa bila kuwahi kusikia kuhusu Yesu au Mtume Muhammad au vitabu vitakatifu, lakini aliishi maisha ya upendo na wema kwa wenzake. Je, ni haki kwa Mungu kumtupa motoni kwa kutofuata dini au kumuamini mtume ambaye hakuwahi kumjua wala kufundishwa habari zake? Kama anaenda mbinguni bila kufuata dini, basi umuhimu wa dini ni nini?
4.Dini zote zinafundisha kanuni ya kimantiki kwamba "kila kitu kilichoumbwa au kilichopo lazima kiwe na muumba au chanzo." Ikiwa tunaifuata kanuni hii ya kimantiki kuwa hakuna kinachotokea bila chanzo, je, Mungu alitoka wapi? Ikiwa jibu ni "Mungu hana mwanzo wala mwisho," kwa nini kanuni ya uhitaji wa Muumba inatumika kwa ulimwengu pekee lakini inavunjwa inapomfikia Mungu?
5.Binadamu anapata maana ya maisha, furaha, na malengo kwa sababu anajua muda wake ni mfupi na ana changamoto za kutatua. Je, kuishi maisha ya raha yasiyo na mwisho au ukomo wowote (trilioni na trilioni za miaka mbinguni au peponi), bila changamoto yoyote, hakutafanya maisha yakose maana au kuchosha?