Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Asante sana mkuuNdio Daladala zinazo toka njia ya buguruni(kutoka g/mboto,Temeke nk) kuelekea Mbezi huwa zinafika mwisho wa mbezi(kama kituo Cha daladala ya mbezi). Ukishafika kituonii hapo upande wa kaskazini Magharibu utaona jengo La stendi hiyo ya Mabasi maan ni kubwa na lina muundo tofaut na majengo mengii(unaeza uka google picha yake kukuona ili upate picha ya utakachotegemea kukiona ukifika) pia utawaona madalali wengi tuu na utaona hata watu wengine wakinaelekea huko maana kuna hitaji kuvuka barabara ya morogoro ili kwenda stendi hiyo.. Kwa ushauri ikiwa huitaji kelele za madalali ukishuka usiwahoji fika sehemu unaona unaeza mhoji muhusika kama vile machinga kukuonesha njia ya kuelekea huko itakusaidia zaidi.
Unataka daladala zima wajue kuwa huyu kaka mshamba. Konda atakupa jibu ambalo hukutegemea.
mtizamo wako tu..binafsi huwa namuuliza konda sijawahi kupata jibu bovu....pengine inategemea na ulivyouliza
Naenda Mafinga sio Shinyanga.
Ni mtu tu kujishtukia, haiwezekani ukafahamu kila sehemu na kila kitu, kuuliza ni muhimu.Hahaa ivi ni kwa nini dar ukiuliza kitu unaonekana mshamba?
Makonda wana ushirikiano mzuri sana wanapoulizwa au kuombwa kuwakumbusha kituo unachoshukia..Unataka daladala zima wajue kuwa huyu kaka mshamba. Konda atakupa jibu ambalo hukutegemea.