Swali kuhusu Bomu la atomic Hiroshima


Sababu kubwa ya kutopiga Ujerumani walikuwa wanaogopa uwezekano wa Ujerumani kuwa na bomu kubwa zaidi ya lile la Kwao. Asilimia kubwa ya scientists waliokuwa kwenye Manhattan project walikuwa wamekimbia kutoka Europe (Oppenheimer, Enrico Fermi...) na walikuwa tayari wameanzisha project ya kuangalia details za atomic reaction. Lakini kumbe waliogopa bure kwani confusion iliyotokana na vita ilikuwa kubwa huko Europe.

Ndipo walipoamua kuyabwaga Hiroshima na Nagasaki and the rest is history.

Kuna kitabu kimoja 'The making of atomic bomb' (nimesahau mwandishi) kimeeleza kwa urefu hadithi nzima ya utengenezaji wa bomu hilo.
 
Majanga ya nayosababishwa na binadamu duniani hayakuanza leo, hapo Marekani cjui tuseme lilikua taifa la kigaidi?
 
Majanga ya nayosababishwa na binadamu duniani hayakuanza leo, hapo Marekani cjui tuseme lilikua taifa la kigaidi?

Kwa hapo sidhani kama utakuwa sahihi kuiita USA kuwa taifa la kigaidi. Hapo ilikuwa ni kipindi cha vita na kama unavyojua vita ni vita tu. Lakini pia tukio hilo ndio lililosaidia vita hivyo (WWII) kuisha mapema !
 
Kwa hapo sidhani kama utakuwa sahihi kuiita USA kuwa taifa la kigaidi. Hapo ilikuwa ni kipindi cha vita na kama unavyojua vita ni vita tu. Lakini pia tukio hilo ndio lililosaidia vita hivyo (WWII) kuisha mapema !

Vita imeisha mapema, athari bado zingalipo!
 
Sijajua picture hii ilipigwa na nani but nimeipenda na kuamua kushare na watu wa nguvu wa JF !

Wakati mjapan anashambulia kambi ya wanajeshi wanamaji kule Hawaii, jeshi la Japan na Marekani yalikuwa na uwezo gani kila moja kwa kuyalinganisha??
 
Mie naona mleta mada kaileta kifolosofia zaidi kuliko tunavyodhani! Nyie subirini!
 
Asante mleta uzi.
Ngoja nimalize majukumu ya bepari, ndipo nikuje na habari za undani kuhusu bomu hili lililoitwa NAGASAKI.
 
Asante mleta uzi.
Ngoja nimalize majukumu ya bepari, ndipo nikuje na habari za undani kuhusu bomu hili lililoitwa NAGASAKI.

Ahsante MKUU kwa kuingia absolute chaka, Hiroshima na Nagasaki ni miji ya Japan iliyopigwa mambomu hayo. Bomu lile lililopigwa hiroshima liliitwa "little boy" ambapo ilikuwa tarehe 6 august 1945 na lile lililopigwa Nagasaki liliitwa "fat man" mnamo tarehe 9 August 1945.
 

Well said
 
kuna mtu alisalimika kweli hapo? duh

-Actually kuna watu walosalimika. Because as you see within the first two to four months of the bombings, the acute effects of the atomic bombings killed 90,000–166,000 people in Hiroshima and 39,000–80,000 in Nagasaki; roughly half of the deaths in each city occurred on the first day !
 
Nagasaki-ni-mji-wa-Japani-kwenye-kisiwa-chaKyushu-mwenye wakazi 450,000.

Umejulikana kimataifa kwa sababu uliharibiwa tarehe-9 Agosti-1945-na-bomu la nyuklia-la Kimarekani-kama mji wa pili katikahistoria-baada ya-Hiroshima.-Bomu-hilo liliua watu 36,000 mara moja na wengine waliokadiriwa kuwa kati ya 70,000 na 100,000 walikufa baadaye kufuatana athira yamnururisho wa kinyuklia.

Kihistoria Nagasaki ilikuwa-kitovu-cha-Ukristokatika Japani mnamo mwaka-1600.-Imanihiyo ilipigwa-marufuku-na-serikali, hivyo Wakristo wengi-waliuawa-katika miaka iliyofuata. Wachache walitunza imani kwa siri hadi kurudishwa kwa-uhuru wa dini-katikakarne ya 19.
 
Mie naona mleta mada kaileta kifolosofia zaidi kuliko tunavyodhani! Nyie subirini!

BOMU la nyuklia ni silaha inayosababisa mlipuko mkubwa sana na ni silaha hatari na yenye nguvu kuliko silaha yoyote iliyowahi kupatwa kutengenezwa katika historia ya silaha duniani.

Mabomu haya ya atomia hutengenezwa kwa kutumia madini yaitwayo uraniamu au plutoni.

Pindi lipigwapo bomu hilo husababisha kuondoa kila inachokikutwa katika uso wa dunia na kugeuza eneo hilo na kuwa jangwa.

Teknolojia ya kufyatua mabomu ya nyuklia
Kuna hasa namna mbili za kufikisha mabomu haya panapolengwa njia ya kwanza ni kutumia ndege za kivita na njia ya pili ni kutumia roketi.

Pia kuna mabomu madogo yanayoingizwa katika makombora ya mizinga.

Nchi ya Japani leo Agosti 6, haitaweza kusahau tukio la kupigwa bomu la Nyuklia katika miji yake ya Hiroshima na Nagasaki ikiwa vita ya pili ya dunia ikielekea kufika ukomo.

Japani ilijikuta ikipata kipigo hicho kitakatifu kutoka kwa Marekani ambayo iliamriwa kufanya hivyo na rais wake Harry S. Truman, kupiga mabomu hayo mfululizo kutokea Agosti 6 hadi Agosti 9, 1945.

Bomu hilo ambalo lilipewa jina la ‘Little Boy’ liliporomoshwa jiji la Hiroshima siku ya jumatatu, Agosti 6, 1945, hadi Agosti 9 likamaliziwa na Nagasaki na kuandika historia ambayo haitasahaulika duniani.

Mlipuko huo hasa ndiyo uliosababisha kupinga utengenezaji wa mabomu ya aina hiyo kwani ulifanya maangamizi makubwa kwa kuua jumla ya watu 140,000 huko Hiroshima na 80,000 wa Nagasaki mwishoni mwa mwaka 1945.

Siku chache baada ya kumalizika kwa tukio hilo inakisiwa kuna asilimia kati ya 15 na 20 ya watu waliopoteza maisha kutokana na majeruha waliyoyapata kutokana bomu hilo.

Wapo waliofariki kutokana na hewa ambayo ilikuwa ya sumu kutoka katika bomu hilo, wengine walikufa kutokana na mionzi yake na wengine kansa.

Kutokana na uwezo wa mabomu hayo siku sita ya kupigwa kwake huko Nagasaki, Agosti 15, Japani ilitangaza salimu amri na Septemba 2 alisaini kuachana na vita hivyo.

Mradi huu uliopewa jina la ‘The Manhattan Project’ ulikuwa wa kwanza kutengenezwa ukiwa chini ya ushirikiano kati ya wataalamu kutoka Marekani, Uingereza na Canada.

Kihistoria mji wa Hiroshima ambao uliathiriwa na bomu la nyuklia ni mji Mkuu wa Mkoa wa Hiroshima.

Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mnamo mwaka wa 2009, mji una wakazi wapatao milioni 1.2 wanaoishi katika mji huu. Mji huu uko kwenye kisiwa kinachojulikana kama Honshu.

Mji umekuwa maarufu duniani kwa sababu ilikuwa mji wa kwanza katika historia iliyoshambuliwa kwa bomu ya nyuklia.

Mji huu ulijengwa upya baada ya vita kuu ya pili ya dunia. Katika mji huu kuna gofu ambalo linajulikana kama ‘Kuba ya Bomu ya nyuklia’ ni gofu la nyumba linalohifadhiwa kama kumbukumbu ya mlipuko, na jengo hilo limeingizwa katika orodha ya urithi wa dunia.

Kabla tya kushambuliwa mji huu ulikuwa na msongamano wa watu waliokuwa wakifikia 381,000 lakini baada ya vita kuisha idadi hiyo imepungua na kufikia kiasi cha watu 255,000.

Mji mwingine ulikumbwa na shambulio la mabomu hayo ulikuwa Nagasaki ambao nao unapatikana katika kisiwa cha Kyushu.

Mji huu nao umejizolea umaarufu kutokana na shambulio hilo la mwaka 1945 na kwa sasa unatumiwa kama mji wa pili wa kihistoria baada ya Hiroshima.

Mji huu ulipopigwa na bomu ulisababisha mauaji ya watu 36,000 hapo hapo na wengine waliokadiriwa kuwa kati ya 70,000 na 100,000 kufariki baadaye kutokana na maradhi yaliyotokana na nyuklia.

Kabla ya angamizi hilo Nagasaki ilikuwa kitovu cha Ukristo katika Japani mnamo mwaka 1600 na imani hii ya Kikristo ilipigwa marufuku na serikali ya Japan.

Agizo hilo la kupigwa marufuku kwa Ukristo ilisababisha wakristo wengi kuuawa katika miaka iliyofuata na wapo walitunza imani hiyo kwa siri hadi kurudishwa kwa uhuru wa kuabudu katika karne ya 19.

Kanisa lililokuwa maarufu la Kikatoriki huko Nagasaki linalojulikana kama, Urakami Tenshudo liliharibiwa na bomu la nyuklia Januari 1946.

Pia katika mauji hayo inadaiwa asilimia 90 ya madaktari waliuawa ikiwa ni pamoja na asilimia 93 ya wauguzi wa Hiroshima.

Inadaiwa kwamba baada ya kupigwa bomu hilo iliathiri mfumo wa mawasiliano na kituo cha redio kilikata kurusha matangazo yake kwa muda wa dakika 20 ikiwa ni pamoja na usafiri wa reli kuacha kuingia katika mji Hiroshima kwa umbali wa kilomita 16.

Nchi ya Japan iliingia hasara kubwa ikiwamo upungufu wa dawa kutokana na watu wengi kuathirika na mabomu hayo.

Wapo watoto waliokuwa wakizaliwa kiajabu wengine wakizaliwa wameungana, na inakadiliwa mwaka 1950 na 1990, asilimia 9 ya watu waliathiliwa na ugonjwa wa kansa na mkanda wa jeshi.

Wataalamu miaka ya 1980 waligundua kwamba iwapo milipuko hiyo ingelipuliwa kwa robo hadi nusu ya silaha za nyuklia zilizokuwepo tayari ingetosha kumaliza maisha ya dunia kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa ambayo ingetokea.

Maradhi haya yangesababishwa kwa kiasi kikubwa na vumbi iliyokuwa ikirushwa hewani na milipuko hiyo ya wakati huo.

Inadaiwa kwamba vumbi hiyo ingejaza anga na kuzuia nuru ya jua kufika kwenye uso wa dunia hivyo kusababisha giza pamoja na kushuka kwa halijoto kwa muda wa miaka kadhaa.

Hatari nyingine ambayo ingeweza kuikabili dunia ilikuwa ikijulikana kama ‘mnururisho wa kinyuklia’.

Hatari hii ilijulikana kutokana na milipuko ya kwanza ya 1945 na majaribio ya baadaye ya kwamba watu na wanyama wamekuwa wakifa kutokana na ugonjwa nururifu wakiathiriwa na kiasi kikubwa cha mnururisho au kupata kansa baadaye kwa wingi.

Mnururisho huo hukaa kwa muda wa miaka katika ardhi pia hukusanyika na mimea hasa katika matunda na nafaka.

Kwa njia hii huathili tena watu wanaotumia mimea hii au wanyama wanaotumia mimea yake kama chakula.

Imekadiriwa ya kwamba milipuko mingi katika vita ya nyuklia ingesababisha kiasi cha mnururisho kitakachobebwa na mawingu na upepo hadi pembe za dunia na kupeleka kifo hata pale pasipo na vita.

Katika vita hii waliokufa kufa hawakuwa wajapan pekee bali pia wakorea wapatao 20,000 walifariki huko Hiroshima na wengine 2,000 walifariki katika mlipuko wa Nagasaki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…