Kama unanunua kitu ili after 1-2 years uuze, basi nunua kitu kingine sio gari. Gari sio asset nzuri.
Tukija kwenye minivans, wengi tunavyonunua tunakua na matarajio positive ila minivans (na MPV) zina watu wake, izo sio daily drives, izo zina matumizi maalumu kama family vacations, etc kutumis hii gari mwenyewe kila siku utaona mzigo kwasababu ni kubwa, ulaji wa mafuta lazima utakua mkubwa ila reliability is too general kusemea.
Kwa Nissan Serena, unaongelea ya mwaka 2005-2015 kweli yana shida. Mostly alternator (na inauzwa bei kinoma alternator yake, jaribu kuulizia kwa dealers), overheating, burning oil, gearbox si unajua CVT ya Nissan majanga..
Sio kwamba ni gari bovu, vyote ivyo vinaweza kuepukika ukizingatia preventive maintenance.