Swali kuhusu tabia ya kususa, kugomea au kuzira: Je, si tabia za kike, si utoto?

Mwanzoni nami nilikuwa na mtazamo kama wako lakini kwa kinachoendelea kuendelea kushiriki ni kuendelea kuhalalisha matumamizi mabaya ya fedha na kuendelea kuidanganya Dunia kuwa tuna democracy. Mi naunga mkono kuachana na hizi chaguzi za viini macho, ila wahusika wasibweteke eti wamesusia, kama ulivyosema nyani ukimsusia shamba la mahindi lazima uvune mabua. Hivyo, wasuse lakini watafute njia muafaka ya kupatikana kwa tume huru kikweli kweli.
 
Naona nimeamka vibaya. Hili ndio kabisa sikuelewi. Kugomea kipenga? Hapa ni kulurunganya kwa kwenda mbele. Huo mchezo wako wa mpira wa vichwa na sio miguu. Au umejibu kama mawaziri watz wakijibu maswali ya wapinzani bungeni! Si amejibu lakini. Haiangaliwi kajibu nini. Bora liende. Wapi? Hakuna ajuaye. Nakuomba jielekeze kwenye hunger strikes kiduchu. Naona kama leo una midadi tosha ya kupakua majibu. You might make my day. Nione yanavyoingia mahubiri yako kuhusu kususa kuwa tabia ya kike au kitoto!
 
Mkuu Ebe, kwenye bandiko langu nimezungumzia kugoma na kususa.
Angalia tarehe ya bandiko hili, usome uone niliandika nini na lini
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020? - JamiiForums
P
 
Kumbe unajua!
Sasa kwa nini unageneralize kama mtu ambaye hajaenda shule?
 
Kwa Kiingereza chako umedai kususa uchaguzi ni Attention seeking. THIS IS VERY WRONG.

SOMA HAPA - Where there is reason to believe that an election will not be conducted fairly or where there is refusal to recognize the authority of the régime conducting the election, an opposition movement may refuse to put up candidates and may urge people to refuse to vote. The aim of such a boycott is usually to protest the use of the election to deceive people as to the degree of democracy present; or it may be an attempt to prevent the "real" issue or issues, as seen by the resistance group, from being overshadowed by "lesser" issues.

Odinga alisusa uchaguzi wa marudio Kenya, je unajua sasa ni nani? Watu waliwahi kususia kuanzia Finland, Urusi, Morocco na kwingineko - hivyo usipuuze maana halisi ya kususia uchaguzi. Pia uache kukebehi wanawake na kudharau watoto.

Hoja zako TANO pia hazina mashiko hata kidogo, ni upotofu tu uliotumwa na mabwana zako katika kujaribu kuwapooza kwani zamani ulijaribu kuwakaanga na sasa unakaangwa - wewe usiye na msimamo.

SOMA MAJIBU HAYA JUU YA HOJA ZAKO MUFILISI
Kususia kushiriki uchaguzi ni suluhisho, wala sio kujiua kisiasa hata kidogo. Kwa sababu tayari zmekwishajengwa hoja madhubuti, lakini watawala hawako tayari kukaa mezani na kuzungumza. Mahakama pia zipo compromised, zimeshindwa kuzifumua sheria kandamizi za uchaguzi ili zituletee uchaguzi huru na wa haki.

1. Tume yetu ya Uchaguzi NEC, haipo huru hata kidogo. Ni tume inayoteuliwa na mwenyekiti wa chama kimojawapo cha siasa. Mahakama pia haziko huru kwa msingi kama huo, hata bunge halipo huru kwa kuwa tumeona pesa zinatumika ambazo hazijaidhinishwa katika bajeti yoyote na hakuna spika wala microphone inayoongea chochote.

2. Mtu anayetekeleza sheria kandamizi kwa kisingizio kuwa sio yeye aliyeitunga hakufanyi sheria hiyo kuwa rafiki. Ni sawa tu na polisi wa makaburu waliokuwa wanaua watu weusi kwa kudai wanatekeleza sheria. Hoja yako ni ya kikaburu zaidi.

3. Chama dola kinaweza kushindana na chama kapuku na kikang’olewa tu amdarakani endapo hakingilii kwa mabavu sauti za watu na kugeuza matokeo. Yaani pamoja na mgombea kuingia na ving’ora bado watu wamekikataa hicho chama chako, sasa chama chako kinatumia ubavu kuzuia transparency! Hii ndiyo hoja, wala siyo mambo ya chama dola vs kapukus. Wapinzani hawashindani na chama dola bali wanashindana na dola yenyewe.

4. Utakubali vipi matokeo ambapo kura zinahesabiwa ukiwa nje ya chumba cha kuhesabu kura zako? Hivi unatumia akili kweli katika hoja hii au mapumba yamejaa kichwani mwako?

5. Asiyekubali kushindwa so mshindani, sasa dola ikubali kuwa imeshindwa na iache kurundika polisi 5,000 kwenye jimbo moja tu ktk uchaguzi mdogo ambao wote tumewaona wakinywa mvinyo baada ya matokeo kutangazwa. Una hoja gani mtumwa wewe!

Kama umeuza utu wako ujue bado tupo tunaouona ukweli na kutaka haki itendendeke. Kama unadhani kususia sio suluhisho, endelea kulala usingizi, utakapoamka utaona matokeo ya strategy hii.
 
Umeeleweka crucifix, tuombe Mungu hii strategy ifanye kazi mapema sana kabla ya 2020..mbali na hapo hali halisi tunaiona....
 
Mkuu the Crucifix, japo bandiko lako ni kweli limeni crucify kupitia crucifixion hivyo mimi kuwa crucified lakini naomba kwanza nikupongeze kwa objectivity yako na kupangua hoja kwa hoja, maana tangu bandiko hili limepanda ile, Feb 19, 2016 na hadi sasa kufikia michango zaidi ya 200, leo ndio nimeona mtu kajibu hoja za maana tena kwa kupangua hoja kwa hoja. Thanks.

  1. Sasa twende kwenye hoja, mdogo mdogo. Wengi wa wachangiaji humu jf ni wishful thinkers and not realists, hata hoja zako kuhalalisha kususa, japo ni justified lakini sio practical kwa mazingira ya siasa za Tanzania, hivyo kwa Chadema kususa ni suicidal. Mimi ni realist, hivyo naeleza kitu cha ukweli kilichopo na kitakachotokea.
  2. Umesema "opposition movement may refuse to put up candidates and may urge people to refuse to vote". kitakachotokea Hii ingekuwa applicable kwenye nchi zenye the opposition movement, it's very unfortunate Tanzania hatuna opposition movement, tuna fragmented opposition, kama Chadema wangeitisha a united opposition na tamko la kususia likajumuisha vyama vyote, that would be something else.
  3. Lakini kwa hali ilivyo, Chadema wakisusa, vyama vingine vitajitokeza na uchaguzi utaendelea to the advantage of CCM, hivyo mwisho wa siku, Chadema ndio wataishia kuwa the biggest loosers kwa kumuachia ngedere shamba letu la mahindi.
  4. Kama CUF ambayo yenyewe ni the opposition movement kule visiwani Zanzibar tena iko kisheria kabisa kuwa SMZ itakuwa ni SUK, CUF waliposusa, na CCM kubaki peke yake, hivyo kungepelekea SUK ishindwe kuundwa, kilichofanyika ni kuwateua watu kutoka vyama vikaragosi na kuunda SUK.
  5. Chadema haijifunzi kwa CUF, nimesema, kuna kugoma na kususa, kugoma ni kwa malengo, kuna something you wish to achieve, lakini kususa ni kuzira with nothing to achieve. By now CUF wanajuta.
P
 
Wanabodi, hata kususia kujiandikisha uchaguzi wa serikali za mtaa ni kususa ni tabia za...
P
 
Vitu vingine ni kama basi la abiria, usiopanda wewe, mwenzio anapanda, na pia ni kama kiti cha basi unaposhuka, anakaa mwenzio.

Wale mnao susa, suseni, ila tambueni ukisusa, wenzio twala..
P
 
Unaishi Tanzania mkuu?! ujenge hoja na nani? Unaweza kujenga hoja au kukaa meza moja ya mazungumzo na dikteta?!Wewe unaweza kwenda kujiandikisha kupiga kura kwenye nchi ambayo ukimchagua mpinzani anatakiwa kuomba msamaha kwa sababu ya kuwa mpinzani?!
 
Wanabodi, hata kususia kujiandikisha uchaguzi wa serikali za mtaa ni kususa ni tabia za...
P
nimaamuzi tu sio lazima huwezi sema watu wamesusa, ila nikwamba hawajaamua maana sio lazima kujiandikisha. hili sio jambo la kumlazimisha mtu wala haina maana ukijiandikisha ww ndio mtanzania wa maana kuliko wengne. ...tuaache watu wapumzike jaman watu wana waza ugali wao
 


Swali zuri Je utacheza mchezo kama unajua matokeo yameshapagwa hata kama ukiwa na uwezo zaidi. Tume ya Tanzania ya sio huru kama wengi wanavyosema mfano Kuna wanasiasa sasa hivi wanaongea na kuwaita wapinzani wadudu na wananchi na viongozi wasifanye kazi na upinzani je wamefanywa nini ? Kwenye demokrasia tumerudi nyuma zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…