Duh...!, laiti ungalijua.
Sijitapi wala sijidai kuhusu numbers ila amini usiamini nikiwa darasa la 7, kwenye school mock exam ya maswali 25, niliongoza kwa kupiga 96%, nilikosa moja, kuna hesabu ya eneo la chombo cha chakula cha kuku, darasa zima walipatia, mimi tuu peke yangu ndio nikakosa.
Baada ya kugaiwa mitihani nikafanya tena likaja jibu lile lile, sikukubali nikamuomba Mwalimu tufanye ubaoni. Nikaitwa nikashusha likaja jibu lile lile langu, akaitwa mwanafunzi mwingine akafanya, jibu likaja lile la waliopatia, mwalimu akauliza darasa, nani kapata, darasa zima wakaonyesha ni yule mwenzangu, wote wakasema nimekosea na nikazomewa.
Kiukweli kwa ubishi mimi mbishi, sikukubali nikaorodhesha kila kipande na kuonyesha jumla ya eneo lake, niko right na wale wengine wote they got it wrong. Wengine wakawa wana nishangaa kwamba nimeongoza hesabu na bado nalalamika, essence ya kulalamika sio kutafuta 100 bali kutendewa haki.
Ndipo mwalimu akakubali hilo swali lifanywe upya ubaoni, likaja jibu langu, mwalimu akashangaa na kujiuliza How could it be, maana jibu la kwenye marking scheme ni jibu lile la wote.
Swali likaja kwa nini darasa zima wamepatia na Mimi Ndio nimekosea, kumbe kuna wenzetu wana Kiongozi cha Mwalimu, walicopy jibu kule kumbe kwenye Kiongozi cha Mwalimu hilo Swali limekosewa!. From then, nilijulikana ni kipanga wao wa hesabu.
Au nikuwekee matokeo yangu ya O level ushuhudie mwenyewe kwa macho misonge iliyonipeleka Ilboru?.
P
Sasa kama ni hivyo mbona huku JF hutumii hisabati? Ila kiukweli mm nakukubali sana na huwa sipendi ukosee