Naomba kufahamu mambo kadhaa kuhusu mkongo wa Taifa:
1. Je umekamilika?
2. Je tumeshaanza kuutumia? Kama jibu ni ndiyo, mbona basi speed ya internet iko vilevile kama zamani na mbona bei hazijashuka kama ilivyotarajiwa?
3. Kama haujakamilika, je ukikamilika kutakuwa na unafuu wowote au ni PROPAGANDA TU?
Najua hapa JF kuna watu wanaojua. Naomba mtujuze tafadhali.
Ahsanteni!
Umeshaanza kutumika kipindi na nafuu ya speed ipo na bei imepungua kwa kiwango kikubwa sana. Kutokuwepo kwa speed naona inategemea na ISP na kiwango cha band-with kilichonunuliwa
Kama nakumbuka vizuri mwaka jana wakati haya mambo yanaiva kulikuwa na optic fiber cable companies/consortiums tatu. Hivyo kam zote zimeanza kufanya kazi ushindani unapaswa kuwepo.Haujakamilika in the sense kuwa zile link za kusambaza nchi nzima bado hazijakamilika.
Bei zimepungua sana angalia package ya Unlimited Voda au bei za broadband ya TTCL sasa hivi ukifananisha na kabla ya fiber.
Nadhani kushuka zaidi mpaka ije cable itakayoleta ushindani maana investment ya kujenga fiber ya baharini ni kubwa sana, so bei haziwezi kuwa low.
Umeshaanza kutumika kipindi na nafuu ya speed ipo na bei imepungua kwa kiwango kikubwa sana. Kutokuwepo kwa speed naona inategemea na ISP na kiwango cha band-with kilichonunuliwa
na sehemu ulipo