Swali: Kuna Mawakili/Wanasheria ambao sio Wasomi?

My point was in Professional Ethics.
1. Kwanza ww umesoma Sheria..??
2. Pili is it true Mtu wa darasa la saba anaweza kwenda kumtetea mtu mahakamani..??
Wewe hujui halafu unataka kujifanya mjanja!!
Hapa umetoa ufafanuzi au umeuliza ili ueleweshwe!??

Sasa unauliza kama mimi nimesoma sheria, shida yako wewe ni kujua taaluma yangu au usahihi wa majibu yangu!??
Hakuna sheria yeyote inayoweka masharti ya viwango vya elimu vya mtetezi(wakili) mahakamani.
Nenda vijijini kwenye mahakama za mwanzo halafu uliza mtetezi wa mtuhumiwa ana elimu gani.
Mimi mzee wangu hata darasa la saba hakufika( aliishia la nne la zamani), lakini watu wakipata kesi walikuwa wanamfuata ili akawatetee mahakamani.
 

Sawa bas ngoja nikufundishe usiendelee kupotosha watu.
The Advocates Act cap. 341 as Amended [2002] inasema hivi.
Kwanza ili uwe Advocate
Section 8(1) A person may apply to the Chief Justice to be adnitted as an advocate
(a) If he holds one of the following qualifications, that is to say
(i) Holder of Degree in Law granted after examination by the University of East Africa or the University of Dar es Salaam or other Institution as my be recognised.
(ii) If he's a legal practitioner and thereby has a right of audience before any court having unlimited jurusdiction in civil & criminal matter in any commonwealth country.
(iii) If he's a solicitor of the supreme court in England, Northen Ireland or the Republic of Ireland.
Mjuni Lwambo tuambie HAPA MTU WA DARASA LA SABA ANAFIT WAP..???

Haya tuje kwenye katazo
Section 41.
(1) No "unqualified" person shall act as an advocate, or agent for suitors or as such issue out any summons or other process or commence or carry on or defend any action, suit or other proceeding in the name of any other person or in his own name in any court of civil or criminal jurisdiction or act as an advocate in any cause or matter, civil or criminal.
Section 42. Imeweka fine ya shilling million moja au kifungo cha miezi 12 kwa mtu atakaye kiuka section 41.
Halafu kwa taarifa yako tu Advocate hasimami Primary Court kisheria mashauri yote ya Mahakama ya mwanzo yanaamuliwa na Sheria inaitwa Magistrates Courts Act 1981 (R.E 2002) na sheria nyngne Shirikishi ambako legal complication ndogo na ndio maana zaman walikua wanachukua mahakimu wenye certificate (Sasa sheria inabadikishwa ku accomodate maadvocate na wameshaanza kuajiri mahakimu wenye shahada ya kwanza.
Mimi sihitaji kwenda kuuliza watu, am among those wa kuulizwa nimekupa legal facts usiongelee mambo ya sheria ki ubishani wa vijiweni njoo hapa na facts hii ni sayar ya wasomi sasa kama ulidhani najifanya mjanja am sorry mimi sipo huko mi nimeona nigusie pale ulipowapotosha watu. Njoo hapa na vifungu vya sheria sio maneno matupu ili watu wapate elimu na sio ubishi huo hauelimishi.
 
mossad007, umenakiri vifungu, Lakini tatizo sio vifungu tatizo ni kuvitafsiri hivyo vifungu.

Hiyo unayozungumzia The advocates Act cap 341 as amendedin 2002 inazungumzia sasa huyo anayeitwa wakili msomi au wakili mwanasheria.

Ukishapata shahada ya sheria, unakwenda shule ya sheria( school of law) baada ya hapo unaandika barua kwa jaji mkuu ili kuidhinishwa kuwa advocate(wakili msomi).

Hayo makatazo pamoja na hiyo faini, ni kuzuia mtu asiye msomi wa sheria(wakili msomi) kufungua ofisi na ku act kama advocate kwa maana ya wakili msomi.

Umesema mwenyewe kuwa primary courts( mahakama za mwanzo)hawaendi mawakili wasomi, anaenda nani sasa?
Hizo kesi zinaendeshwa bila kuwa na upande wa utetezi?

Needless to add, an advocate(wakili) is a who argue for a cause of another person, who speaks or write in a favor or support of another person(regardless of his education).

Halafu usitusahaulishe ajenda kuu, tuambie kwa nini mtu anaitwa wakili msomi, ina kuna wakili mwingine sio msomi??
 

1. Kwanza Shule ya Sheria haiitwi "School of Law" inaitwa Law School ungekua mwansheria ungejua tofauti ya the two phrases.

2. We mtoto nimekua wakili kwa miaka 4 sasa mambo ya wakili msomi sio sheria wala haiko subjective na mambo ya sheria huu ni utamaduni tu wa kuitana kwa heshima kama Legal Ethics inavyotufundisha ndio maana nikakuuliza umesoma sheria..?? kwa sababu unaleta point za vijiweni ubishi ambao huwezi kuta wanasheria wanabishana mambo haya .
Nikujibu sasa!
3. Neno wakili (Advocate) kwenye context ya Sheria lina maana tofauti likitumika pia kwenye context nyngne.
Advocate kwenye Sheria ni mtu anayesimamia kesi kwa niaba ya mtu mwingne (mteja).. advocate inaweza ikawa verb pia yani kurecomend or support kwa kiswahili tunasema kuhamasisha mfano kuadvocate vijana kuacha matumizi ya madawa ya kulevya. Sasa unaposema Advocate msomi hii ni legal recognition tunayofundishwa kwenye Legal Ethics (likely wewe hujasoma cz sio mwanasheria) kua among the duty of a lawyer to a fellow lawyer ni respect na hii tumeiridhi kutoka kwa waingereza wao ndio wametuletea huu utamaduni wa kuitana learned sister/brother au Lordship kwa Majaji. Wala sio kitu kikubwa kama unavyotaka kukionesha hapa.
Mahakama ya mwanzo mashauri huendeshwa kwa pande zote kujitetea wenyewe na ndio maana hakuna serious sentence. sasa utuambie ww BABA YAKO ANASIMAMA KAMA ADVOCATE KWA SHERIA GANI mi nimeshatoa sheria inayokataza na wewe tupe inayompa mamlaka..!!!!
Sheria imesema wazi ili uwe Advocate unahitaji kua na sifa hizo nilizokuonyesha S. 8 sasa wewe BABA YAKO Darasa la Saba hajafika inakuwaje anakuwa Advocate hili swali mbona hujibu...???? unachokwepa ni nn hasa..??
Mwisho nikufundishe sio kila Mwanasheria ni wakili kama unavyowapotosha watu... iko hivi:-
1. Unapomaliza Shahada ya kwanza unatunukiwa LLB hapa unaitwa mwanasheria.
2. Ukifuzu na kufaulu mafunzo ya Sheria kwa vitendo yanayotolewa na Law School of Tanzania hapa ndio unapewa Practising Certificate kwa mujibu S. 8 (3) ya Adv. Act. hapa ndo unaitwa wakili.
Ukumbuke wakili proffessional holder wa professional body

Unaweza ukatoa majibu ya maswali yangu ukisuport na vifungu vya sheria kama mimi nnavyokujibu manake vifungu havidanganyi na maneno matupu ni ujanja ujanja ambao hapa hauna nafas...!!
 
Good!!
Argument yako ni nzuri isipokuwa tu umeni misquote sehemu moja, Hakuna sehemu nimesema mwanasheria ni lazima awe wakili na nimelikanusha hili from the very begining kwamba Mwanasheria anaweza asiwe wakili, otherwise i can just wish you Goodlucky in your advocate activities.
 
Karibu chief.. anytime!
More explainations Mossad, hiyo sheria unayozungumzia inazuia asiye na Taaluma ya uwakili kusimama kuanzia magistate court, high court na court of apeal, haijazuia kwenye primary courts, vipi hapo?
 
LL.B is a noble proffesion
ndo jibu lako..si umeuliza ni kwanini

 
More explainations Mossad, hiyo sheria unayozungumzia inazuia asiye na Taaluma ya uwakili kusimama kuanzia magistate court, high court na court of apeal, haijazuia kwenye primary courts, vipi hapo?

Niwekee hapa hicho kifungu twende sawa..!!
 
wanahaki ya kuitwa wasomi maana wao kazi yao pia ni kusoma kila mara kunasheria zinakuwa repealed na revised na pia kuna case mbalimbali zinatolewa hukumu na mambo mengi sana wanahitaji kusoma muda wote ilikuwa current.
Kwani teknolojia haibadiriki..??? Kama hiyo ndo reference basi wote ni wasome, maana hakuna fani iliyobaki vilevile toka ilipoanza hadi leo
 
Umemuelewa kwamba ni mpotoshaji?

Hapana, Sijamuelewa Kwa Upotoshaji, Mimi Ni Illiterate Kwenye Law, Na Nimeleta Huu Uzi Ili Tupate Kuelimika Na Nina Amini Kuwa Hata Wewe Umeelimika Pia, Suala Nikuchukua Mabandiko Yote Na Kuchambua Kutokana Na Hoja, Wewe Unayejua Inabidi Uje Na Hoja Alafu Tuzipime
 
mwanasheria yeyote sio lazima awe wakili ila wakili lazima awe mwanasheria. Na kitu kingine sio kila mtu anaweza akawa wakili yaani akamtetea mtu mahakamani mwenye mamlaka ya kumtetea mtu ni wakili tu hao wengine mnawaongelea labda walienda mahakamani kutoa ushahidi au hiyo kesi haikusikilizwa mahakamani.
 
Umeielewa lakini hiyo doctrine of Negligence?

Au umekurupuka ukijua unamjibu Layman?

Hahahah usinipimie kirahisi dadayangu activisister mimi ni MWANASHERIA MSOMO! mpigamsuli locuta est causa finita est
 
Na kitu kingine sio kila mtu anaweza akawa wakili yaani akamtetea mtu mahakamani mwenye mamlaka ya kumtetea mtu ni wakili tu hao wengine mnawaongelea labda walienda mahakamani kutoa ushahidi au hiyo kesi haikusikilizwa mahakamani.

Je, watu hawawezi kujitetea wenyewe mahakamani?

Manake kuna jurisdictions si lazima mtuhumiwa atetewe na wakili mahakamani. Mtuhumiwa ana uamuzi wa kutafuta wakili wake, ana uamuzi wa kukubali wakili wa kupewa na serikali, na pia ana umauzi wa kujitetea mwenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…