Swali kwa CHADEMA: Lini rufaa za akina Halima Mdee na wenzake 18 zitasikilizwa?

Baada ya uchaguzi mkuu 2025. Watasikilizwa au kusamehewa ili wawe wanachama
 
Swala hili limechukuwa muda sana kushughulikuiwa lakini naamini watalitolea ufumbuzi soon
 
Sijui kwanini dharura ileile isitumike kuitisha Baraza Kuu na kuifunga hii saga once and for all?

Political science!
 
Siasa unaijua vyema mkuu, hongera... Watu wanadhani siasa sijui ni nini... Siasa ni biashara nzuri tu kama biashara zingine
 
Jamaa bado yupo sahihi, hapo juu alikuwa anaonesha ni kwa namna gani licha ya wale wanawake kukata rufaa bado wao sio wanachama tena wa Chadema, walishafukuzwa.

Lakini kwenye bandiko lake la leo, anataka kujua nini hatma ya hizo rufaa, baraza kuu litakutana lini kwa ajili ya kusikiliza hizo rufaa, licha ya hizo rufaa kutoharibu uamuzi wa awali wa kuwafuta uanachana hao wanawake uliokwisha tolewa.
 

We unazitakia nini?
 
Mkuu, ubarikiwe sana kwa uelewa wako
 
Alafu Bado wanakausha makoo kung'ang'ania katiba mpya, wakati Yao tuu yanawashinda
 
Fact kabisa
 
Wewe kama mwanasheria, Halima na genge lake ni wanachama wa CHADEMA au siyo wanachama? tuanzie hapo
 
Hata kwenye daftari la chama hawapo
 
Wewe kama mwanasheria, Halima na genge lake ni wanachama wa CHADEMA au siyo wanachama? tuanzie hapo
Nilishasema humu humu kuwa kwasasa wote hao si wanachama wa CHADEMA. Ndiyo maana wamekata rufaa kupigania uanachama wao. Lakini, wamekata rufaa ili wasikilizwe. Wasikilizwe na suala lao limalizwe.
 
Nilishasema humu humu kuwa kwasasa wote hao kwasasa si wanachama wa CHADEMA. Ndiyo maana wamekata rufaa kupigania uanachama wao. Lakini, wamekata rufaa ili wasikilizwe. Wasikilizwe na suala lao limalizwe.
Limalizwe wapi mkuu? Maana kwa unavyoongea ni kama suala la uanachama wao ni la kitaifa hivi, wakati ni la binafsi na suala la 'ubunge' wao ndio la kitaifa, lakini halihitaji maamuzi ya rufaa kutekelezwa.
 
Limalizwe wapi mkuu? Maana kwa unavyoongea ni kama suala la uanachama wao ni la kitaifa hivi, wakati ni la binafsi na suala la 'ubunge' wao ndio la kitaifa, lakini halihitaji maamuzi ya rufaa kutekelezwa.
Likimalizwa CHADEMA litamalizwa kitaifa pia. Wanalipwa pesa za umma wale Mkuu
 
Amkeni Amkeni Kumekucha!!!!πŸ˜πŸ™„πŸ˜ΆπŸ˜‘πŸ˜πŸ˜
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…