Vikao vya baraza kuu la Chadema huitishwa kikatiba na sio takwa la mtu au mihemko ya kisiasa, CHADEMA ni taasisi makini na imara. Soma katiba ya Chadema utaelewa.
Kamati kuu ya CHADEMA ilishamaliza kazi yake ya kuwavua uanachama wale Covid 19, ni haki yao kukata rufaa kwenye baraza kuu, na sio kazi ya mwenyekiti au kamati kuu kushinikiza au kulazimisha kikao cha baraza kuu kiitishe, kamati kuu haipaswi kupreempty maamuzi ya baraza kuu, hivyo rejea kasome katiba ya CHADEMA.
Kukumbusha tu, hao Covid 19 sio wanachama wa kwanza wa CHADEMA kuvuliwa uanachama na kwenda kukata rufaa kwenye baraza kuu, Zitto naye alifanya hivyo hivyo wakati akifukuzwa CHADEMA.
Yote kwa yote, hata baraza kuu likitupilia mbali rufaa zao, bado spika na serikali ya CCM itaendelea kuwatambua Covid 19 kama wabunge halali na kuwalipa pesa, ndivyo watawala wa CCM walivyodhamiria hivyo, na lolote liwe. Hivyo Chadema hawana muda wa kupoteza kucheka na malaya wa kisiasa, malaya wa kisiasa wanajijua na wanajua wapi pa kwenda kujiuza!!