swali kwa kina kaka wenye wapenzi

swali kwa kina kaka wenye wapenzi

kama nimevutiwa sana nae na najua tabia zake na nina huakika ni bikra ,dawa nikuchapa nje tu mpaka atakapokuwa tayari kuachia tunda plus tabia zake nzuri na elimu kwamba tutakuwa tuko tayari kuanza maisha.
 
Pole sana bwana VIPER. Mi nakushauri uwe na subira na mwenye uvumilivu. Ila kuna kitu kinatakiwa ukifanye sasa. Inatakiwa uwekeane mkataba na huyo dada kuwa iwapo hautakuta BIKRA pindi utakapomuo ni hatua zipi zichukuliwe?? (kwa mfano kuvunjika kwa ndoa iwapo imani ya dini yanu inaruhusu kuachana baada ya kuoana).
Ili kupunguza matamanio ya kufanya ngono nakushauri uwe unafanya mazoezi ya viungo na wee ni Muislam basi jenga tabia ya kufunga funga za sunnah (Mtu Muhhamad (rehma na amani za Mola zimwendee) amesema kuwa: "Oeni katika wake muwapendao, na kama mkikosa cha kuolea (mahari) basi fungeni kwani kufunga kunapunguza matamanio ya kuzini).
Kitu ambacho unatakiwa ukielewe ni kuwa kadiri ulivyo wee ndivyo hivyo hivyo alivyo huyo mwenzio. Yaani kama wee ni bikira basi uwezokano wa huyo mwenzio naye kuwa bikira ni mkubwa pia. Kwa hiyo wee kuwa mvumilivu tu na umtunzie mwenzio tunda lake naye atakutunzia. Lakini ukianza kuchakachua basi ujue nae atachakachuliwa na wengine. Kitakachofua ni kupewa bikira ya kichina.
:focus:
 
Bacha hujatulia, unahitaji kupepewa!!!!!!!

unajua ni nini kiongozi ,hebu tujaribu kuwa wawazi tu,kama wana ndoa wanatoka nje ya ndoa yao,sembuse huyu mshikaji na demu wake???????yeye ampotezee kwa muda wakati kiu yake anaitafutia njia mbadala!
 
Msimamo wa huyo dada ni mzuri kwa kuwa wewe upo mbali na hawezi kujiachia tu kwako hata kama anakupenda maana anaogopa kubwagwa siku akigundua umepata wmingine huko ulipo.
 
unajua ni nini kiongozi ,hebu tujaribu kuwa wawazi tu,kama wana ndoa wanatoka nje ya ndoa yao,sembuse huyu mshikaji na demu wake???????yeye ampotezee kwa muda wakati kiu yake anaitafutia njia mbadala!
Unishi kwa kufuata wenzio?kama wanandoa wanatoka nje ni lazima awaige?
 
jibu liko wazi kabisa hapo, tena shukuru umeapata mwanamke wa maana, anaonekana anakuzi akiri, kama umeona umeshindwa kumshawishi maana yake nini?? huna uwezo, kwa kukusaidia tu alichokuambia ni sahihi kabisa na anaonekana mwanamke wa msimamo thabiti, atakuwa msaada mkubwa kwako, wewe mwambie siku mkioana itabidi umfanyie test ya wataalamu waliobobea, shangazi zako ili kuhakiki, ikiwa tofauti
vunja ndoa hiyo ya uongo...
 
Nadhani kuna siri Imejificha hapo. Yawezakuwa Dem si bikira kama adaivyo [ anawaza sasa itakuwaje ukigundua], mimi nionavyo kwa hali ya sasa kama dem angekuwa ana future plan na wewe angekupa tunda fasta, ikiwezekana haka kaujauzito ili aku retain. and kwani yeye hajui anapo kunyima tunda wewe lazima unajipoza somewhere,

Sikiliza moyo wako, umvumilie kama unataka mateso otherwise changanya kwato cause mapenzi now days yapo tuuuu, and wapo best partners, all you need is time and chances.

Niliwahi kuwa kwenye sama situation bt in those secondary days, kimsingi mtoto nikamkosa and msela mwingine kabisaa ndo akaopoa, Kuna issues si rahisi sana kuelewa like why akufanyie hivyo and possibly amesha megwa na kamtu fulani (mnisamehe kusema kamtu) kimsingi as you are looking for a partner la personality kana matter so ukiona anamegwa na mtu below your status usishangae...........thats the way it is....
 
UKIFIKIRIA MADEMU WENGI UMEWAKATAA KUSEMA UKWELI KWA KUMTUNZIA HESHIMA YEYE LAKN NAONA NAMNA GANI.
WEWE KAMA RIJALI na Una matamanio UTAFANYAJE ??! na bint kama kuolewa hataki mpaka baada ya miaka 3 ya degree yake ikiisha? UTASUBIRI? !! UTAENDELEA KUMTUNZIA HESHIMA DEMU WAKO AU?!

Msubiri tu kama huna 'plan B'! Ila kama unasubiri kuwa makini sana na ni vema mkaelewana hivyo kwamba unamsubiri yeye. Nje ya hapo kama anasema tu 'atakuwa tayari kuolewa akimaliza degree' kwangu mimi hii sentinsi haipo specific vya kutosha kukupa wewe comfort ya kumsubiri.
 
Unishi kwa kufuata wenzio?kama wanandoa wanatoka nje ni lazima awaige?

unajua nini mama,najaribu kuangalia uzito wa jambo lenyewe!sio kwamba awaige wanandoa kwa kutoka nje!yeye aawe simple tu, kiu yake apeleke kwingine amsubiri huyo malkia muda wake atakaposema YES!
 
Jamani, msihalalishe ngono, kufanya tendo la ndoa nje ya ndoa hakukubaliki. Mimi namuunga mkono huyo dada na namshauri huyo kaka awe mvumilivu, kama mna mawasiliano mazuri utajua tu kama mwenzio ana uhusiano na mwingine.

Mimi ni Mama na nina familia yangu kwa sasa, lakini niliweza kukaa miaka 27 nikiwa bikra mpaka nlipoolewa. Naamini ni heshima kubwa sana mwanamke akiweza kujitunza mpaka aolewe na naamini hata mme akimkuta mke Bikra atafurahi na anajiamini zaidi.
 
mmmmmmh!mpaka 27yrs?wewe ya kwako haikutoka kwa kuendesha baiskeli kweli?
 
Mimi ilinitokea kuwa na "mpenzi" ambaye tuliahidiana kuoana mara nitakapomaliza masomo (miaka 7)! Huwezi kuamini tuliandikiana barua (enzi zile za barua!!), kwa miaka yote hiyo 7, na kwenye kumalizia barua tuliandika "I keep my promise" kwa maana kuwa aliniahidi kunisubiri miaka yote 7!!!! Nilijipa moyo! Cha ajabu niliporudi mawasiliano yalikatika! Baada ya miaka mitano (tangu nirudi) nilioa dada mwingine, ambaye niko naye hadi leo! Siku moja nikakutana na "shemeji yangu" (mdogo wa yule mpenzi wa awali" akaniambia DADA YAKE ALISHAOLEWA! Kwa hiyo conclusion yangu ni kwamba, ningeachwa kwenye mataa! Ushauri wangu kwako Viper, tafuta mchumba UOE! Inawezekana sio ubavu wako huyo!
 
Jamani, msihalalishe ngono, kufanya tendo la ndoa nje ya ndoa hakukubaliki. Mimi namuunga mkono huyo dada na namshauri huyo kaka awe mvumilivu, kama mna mawasiliano mazuri utajua tu kama mwenzio ana uhusiano na mwingine.

Mimi ni Mama na nina familia yangu kwa sasa, lakini niliweza kukaa miaka 27 nikiwa bikra mpaka nlipoolewa. Naamini ni heshima kubwa sana mwanamke akiweza kujitunza mpaka aolewe na naamini hata mme akimkuta mke Bikra atafurahi na anajiamini zaidi.

heshima yako mama HOPE! hongera saana! kama kwelii..
 
Back
Top Bottom