Swali kwa maafisa kilimo na ufugaji

Swali kwa maafisa kilimo na ufugaji

masanzu

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2013
Posts
605
Reaction score
217
nahitaji kuanzisha ufugaji wa kuku wa kienyeji naomba ushauri wa kitaalamu KUKU 100 WANAHITAJI ENEO KUBWA KIASI GANI
 
Mimi sio mtaalam sana ila ni kama 20 metre square kwa kuku 100, ikimaanisha kuku 6 watahitaji 1 square metre.....
 
Mimi sio mtaalam sana ila ni kama 20 metre square kwa kuku 100, ikimaanisha kuku 6 watahitaji 1 square metre.....

Hao kuku sita wa kukaa 1m sq ni kienyeji au hawa wa kizungu? Kama ni wa kienyeji hasa basi inabidi ufugie ndani.

Labda nirudi kwa mwenye swali, unataka kuwafugia ndani au nje?, maana waweza wafugia nje na ukaweka fence ili wasitoke zaidi ya eneo unalotaka.
 
Malila namaanisha 1 square metre, na ni wa kienyeji/ hata wa mayai pia
wanaweza kukaa kwa kipimo na eneo hilohilo.....
Isipokua itategemea na mazingira na muundo au ujenzi wa banda mfano kwa Dar es salaam itabidi wawe kuku 4 hadi 5 kwa sq metre na banda liwe na madirisha ya kutosha kuwaepusha kuku na joto kali.....
 
mi ninataka kuweka fensi ili wasizagae na waishi kama vile wanavyofugwa kienyeji tofauti ni kutozagaa
 
Asante,

Hapa tunaweza changanya maneno, ukitaka kufuga kuku wa kienyeji kizungu maana yake ndio hiyo ya kumpangia ukubwa wa eneo la kujidai huyo kuku wako na umpe chakula chote pale pale alipo. Lakini kienyeji ninachoamini mimi ni kumfuga huyu kuku ktk eneo ambalo limewekwa fence na ana uhuru wa kuzunguka zunguka huku akitafuta chakula na wewe kwa muda uliopanga unampa chakula. Njia hii ni nzuri na salama kuliko ile ya kuwaacha huria kama wafanyavyo vijijini. Sijaona shamba la hivi kwa hapa Dar, ipo haja ya kulianzisha ili liwe shamba darasa.

Mfano, nawafungulia asubuhi wanazunguka bustanini, kisha saa nne nawapa chakula na maji, na jioni nawapa chakula kidogo na maji. Kwa nilivyomwelewa mtoa maada, ni kwamba anataka kujua sasa, kuku 100 watahitaji eneo la hivi lenye ukubwa gani?
 
mi ninataka kuweka fensi ili wasizagae na waishi kama vile wanavyofugwa kienyeji tofauti ni kutozagaa

Mpango wako ni kuwa na kuku wangapi, maana ukishaanza kufuga watazaliana, kwa hiyo kipimo ulichopewa kitakuwa outdated.

Naamini ukitumia hesabu ya mdau hapo juu itakuwa poa sana, yaani kuku sita kwa kila sq meter moja. Kwa hiyo iwe 100/6 unapata sq meter 16. Ili kuwa salama zaidi ongeza sq meter 4 hivi ili kuku wajinafasi. Hii hesabu ni kwa mujibu wa mdau hapo juu, sio mimi.
 
Good idea bro unahitaji kutumia mfumo gani kufugia kuku pia nakushauri utafute jogoo la kisasa ili uboreshe mbegu mi ndo fani yangu bro
 
Good idea bro unahitaji kutumia mfumo gani kufugia kuku pia nakushauri utafute jogoo la kisasa ili uboreshe mbegu mi ndo fani yangu bro

Kama una mtaji, tafuta shamba eka moja hivi, zungusha fence, kisha jenga mabanda ndani ya hiyo fence ili kuku wawe ndani lakini wakiwa na eneo kubwa la kujidai.
 
Nimesha andaa nusu hk lakini nahitaji elimu kama kuna yoyote anajuwa VITABU ELEKEZI vinapatika wapi aniambie kw dar
 
Back
Top Bottom