Swali kwa mabinti / wanawake

Swali kwa mabinti / wanawake

Joss

JF-Expert Member
Joined
May 28, 2009
Posts
765
Reaction score
191
Habari zenu !

Natumaini wote mnapenda wapenzi wenu wawe na sifa zote mnazozihitaji,
Swali langu ni kuhusu sifa mbili kati ya nyingi za mwanamme.
Kuna wanaume wawili, mmoja ni mwaminifu,hawezi kutembea nje lakini hajali sana,hana lugha tamu ya kubembeleza,na pia hawezi kujizuia hasira pale unapomkwaza.
wa pili ni yule ambaye anajali sana,maneno matamu, mstaarabu mwenye kukufanya ucheke na ujisikie unafurahi unapokuwa naye, lakini wakati mwinigine hajatulia, anaweza kutoka nje na wanawake wengine.

Kati ya hao wawili, ni yupi rahisi kumvumilia na kudumunaye katika mahusiano ?

Asanteni !!
 
Mi mtazamaji maana hiki choo sistahili!
 
Habari zenu !Natumaini wote mnapenda wapenzi wenu wawe na sifa zote mnazozihitaji,Swali langu ni kuhusu sifa mbili kati ya nyingi za mwanamme.Kuna wanaume wawili, mmoja ni mwaminifu,hawezi kutembea nje lakini hajali sana,hana lugha tamu ya kubembeleza,na pia hawezi kujizuia hasira pale unapomkwaza.wa pili ni yule ambaye anajali sana,maneno matamu, mstaarabu mwenye kukufanya ucheke na ujisikie unafurahi unapokuwa naye, lakini wakati mwinigine hajatulia, anaweza kutoka nje na wanawake wengine.Kati ya hao wawili, ni yupi rahisi kumvumilia na kudumunaye katika mahusiano ?Asanteni !!
pia kuna kundi la tatu, hawa ni wanaume wenye gubu, wenye wivu, choyo, masimango na roho mbaya.Akiota usiku kuwa una bwana ofisini kwako kesho anakuja kazini kwako na kuanza kukuminia matusi mbele ya staff wenzako.
 
Kwani wewe unaweza kumvumilia yupi? Maana wewe ndio mlengwa!!!

Maneno mazuri, kubembelezwa, lakini jamaa anakula mizigo nje.... tehe tehe tehe,, haina maaana mwanakwetu
 
kuna kundi la nne, hawa ni wanaume waliobalance makundi yote matatu hapo juu....
nyama ya ulimi kiasi, wivu kiasi, charming kiasi, ucheche kwa mbali.
 
Nimekuzimikia ghafla BabyGal
acha hizo huyu kajiunga leo hata ukaribisho bado utamzimiaje? umemfahamu lini? acha papara... well kwenye mada hizo tabia zao zinavumilika kama ukimrekebisha kwa upole na busara
 
acha hizo huyu kajiunga leo hata ukaribisho bado utamzimiaje? umemfahamu lini? acha papara... well kwenye mada hizo tabia zao zinavumilika kama ukimrekebisha kwa upole na busara
Wivu mpaka kwenye kiibodi?!Hatari hii sasa!
 
Do you know why he keeps following you around? Your avatar says it all! Inamvutia!he is imagining you through your avatar!
Hahahaha!Kama ni kweli basi aendelee tu maana uzuri wote upo hapo!
 
Habari zenu !Natumaini wote mnapenda wapenzi wenu wawe na sifa zote mnazozihitaji,Swali langu ni kuhusu sifa mbili kati ya nyingi za mwanamme.Kuna wanaume wawili, mmoja ni mwaminifu,hawezi kutembea nje lakini hajali sana,hana lugha tamu ya kubembeleza,na pia hawezi kujizuia hasira pale unapomkwaza.wa pili ni yule ambaye anajali sana,maneno matamu, mstaarabu mwenye kukufanya ucheke na ujisikie unafurahi unapokuwa naye, lakini wakati mwinigine hajatulia, anaweza kutoka nje na wanawake wengine.Kati ya hao wawili, ni yupi rahisi kumvumilia na kudumunaye katika mahusiano ?Asanteni !!
Sijaona bado.
 
pia kuna kundi la tatu, hawa ni wanaume wenye gubu, wenye wivu, choyo, masimango na roho mbaya.Akiota usiku kuwa una bwana ofisini kwako kesho anakuja kazini kwako na kuanza kukuminia matusi mbele ya staff wenzako.
aina hii ndo funga kazi!
 
Asanteni wadada, kwa hiyo kifupi ni kuwa anatakiwa awe na sifa zote muhimu, jambo ambalo ni gumu kiasi.
 
Back
Top Bottom